Na Mwandishi wetu.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya NchiJumanne A. Sagini amefanya ziara mkoani Mara kwa kutembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ofisi zaChama cha Mapinduzi Mkoa wa Mara pamoja nakukutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama jimbonikwake Butiama.
Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Ali Salum Hapi na Kamati ya Ulinzi naUsalama ya Mkoa huo, Sagini amesema kuwakwa nafasi yake ya Naibu Waziri wa Mambo yaNdani ya Nchi, jukumu lake kubwa ni kuhakikishausalama na amani ya nchi. Ameitaka Kamati yaUlinzi na Usalama kuendelea kushirikianakudhibiti uhalifu unaojitokeza.
Naibu Waziri Sagini aliyasema hayo jana, 21 Januari 2022 alipotembelea Ofisi ya Mkuu waMkoa wa Mara, Wilaya ya Musoma, mkoani Mara katika moja ya ziara yake.
“Moja ya changamoto ninayolenga kuidhibiti nimatukio ya uhalifu yanayojitokeza mara kwa maraMkoani Mara na nchini kwa ujumla, hivyo navitakavyombo vya usalama kuongeza nguvu zaidikutokomeza matukio hayo.
Aidha Naibu Waziri Sagini ameshangazwa nakauli za baadhi ya wananchi wanaosema uhalifuutarudi kwa kasi kwasababu ya mawaziri wapyawa Mambo ya Ndani ya Nchi. Anasema IGP hajabadilishwa, Makamanda wa Polisi Nchi nzimani wale wale, sasa uhalifu utaongezeka kivipi?
“ Kuna maneno yanayosemwa kwamba uhalifuutarudi kwa kasi sasa hivi, naomba niwatoe hofukwani IGP ni yule Yule, Makamanda wa Polisi niwale wale, amani na usalama wa nchi utazidikuimarika”
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mh, Ally SalumHapi amefurahia kwa ujio wake na kuahidi kutoaushirikiano unaohitajika katika kila sekta navyombo vya usalama vilivyomo katika Wizara yaMambo ya Ndani ya Nchi kwenye Mkoa wake.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment