RC SINGIDA AKEMEA MAUAJI YA BODABODA, ATOA MILIONI 2 KWA KIKUNDI CHA VIJANA | Tarimo Blog

Mkuu wa Mkoa wa Singida  Dk. Binilith Mahenge akimkabidhi Mwenyekiti wa Kikundi cha Iguguno Youth Group , Vicky Mwaisakila Sh.2. Milioni alizowaahidi hivi karibu kwa ajili ya shughuli za ujasiriamali wakati wa ziara ya siku moja ya kukagua ujenzi wa miradi ya barabara wilayani Iramba. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo.



Na Dotto Mwaibale, Singida

MKUU wa Mkoa Singida Dk. Binilith Mahenge amewataka wananchi wa mkoa huo kuchukua tahadhari kwa watu wasiowafahamu wanaofika kwenye maaeneo yako na kuwatilia mashaka.

Mahenge alitoa ombi hilo aliposimama kwa muda kutoa pole kwa wafiwa wa Iddi Hassan (25) mkazi wa Iguguno wilayani Mkalama mwendesha bodaboda ambaye aliuawa kwa chomwa na kitu chenye ncha kali mgongoni na tumboni na mtu asiyejulikana ambaye alimkodi.

Dk. Mahenge akizungumza jana na wananchi wa eneo hilo wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja wilayani humo aliwaomba wachukue tahadhari kwa kujilinda, kutoa taarifa na kuwa waamgalifu kwenye maeneo yao wanayoishi.

Akitolea mfano moja ya tukio lililotokea hivi karibuni Kata ya Nduguti wilayani humo ambapo mtu mmoja aliyejitambusha kuwa amefika katika kata hiyo kama muajiriwa wa Jeshi la Polisi ambaye alipanga katika nyumba moja ya kulala wageni akiwa na mwanamke aliyedai ni mke wake.

Alisema mtu huyu alikuwa akimtumia mwendesha bodaboda mmoja kumpeleka maeneo tofautitofauti na baada ya kuona amekwisha mzoea wakati wakinywa chai alimwambie amuachie pikipiki yake ili aende kuripoti kituo cha polisi kuhusu kuanza kazi ambapo alimruhusu kuondoka na pikipiki yake na kutokomea nayo kusikojulikana na walipoenda nyumba ya kulala wageni walimkuta na huyo mwanamke aliyedai ni mke wake amekwisha ondoka.

"Vyombo vya ulinzi na usalama vitahakikisha watu wote waliofanya tukio hilo watakamatwa na kufikishwa kwenye mkono wa sheria" alisema Mahenge.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ikulu ambacho alikuwa akiishi kijana huyo Christina Lema alisema wamesikitishwa sana na tukio hilo kwani marehemu alikuwa hana ugomvi na mtu yeyote na alikuwa akishirikiana na waendesha bodaboda wenzake kwenye shughuli zao.

Alisema kijana huyo alifariki katika Hospitali ya Mkoa Singida alikopelekwa kupata matibabu akitokea Hospitali ya Romani Katoliki katika kata hiyo baada ya kujeruhiwa na mtu huyo asiye julikana ambaye alimkodi na baada ya kufanya unyama huo aliondoka na pikipiki yake. 

Wakati huo huo Dk. Mahenge ametoa Sh. 2 Milioni kwa Kikundi cha Iguguno Youth Group alizo ahidi kuwapa ambapo na aliyekuwa Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa       (OR-TAMISEMI) na sasa Wizara ya Afya Ummy Mwalimu alitoa ahadi ya kiasi hicho cha fedha.

Alitumia fursa hiyo kuishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kwa kutoa fedha na kuwakopesha vijana hao kupitia asilimia 10 zinazo tolewa kwa vijana, walemavu na wanawake na akawaomba wataalamu wa wilaya hiyo kuwa jirani na vikundi hivyo ili kufundisha namna ya bidhaa zao kuwa bora na kuzitofautisha na watu binafsi.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo aliwaasa vijana wilayani humo kuendelea kutumia vizuri misaada na mikopo wanayoipata kupitia wahisani mbalimbali ambayo itasidia ukuaji wa vikundi Kizigo amemuhakikishia mkuu wa mkoa kwamba vikundi hivyo vimejijengea utamaduni wa kurudisha fedha wanazo kopeshwa kwa wakati hivyo kujijengea uaminifu mkubwa katika wilaya hiyo. 

 Mwenyekiti  wa kikundi hicho Vicky Mwaisakila ameishukuru Serikali ya Mkoa na Halmashauri ya Mkalama kwa namna ambavyo wamekuwa wakisaidiwa kufikia malengo yao na kuahidi watatumia fedha hizo vizuri na  matunda yake yataonekana. 

Hata hivyo Mwaisakila ametoa wito kwa vijana kuondoa woga Katika kujaribu kubuni miradi ambayoutawasaidia kuinua kipato na kuleta ajira kwa vijana.

Vijana wa Iguguno Youth Group wakiwa kazini.
Kikundi cha Iguguno Youth Group , Vicky Mwaisakila akionesha fedha Sh.2. Milioni walizo kabidhiwa na mkuu wa mkoa.
Baadhi ya Vijana wa Iguguno Youth Group wakiwa katika picha ya pamoja.
Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Iguguno wakiwa msibani nyumbani kwa Kijana Iddi Hassan mwendesha bodaboda aliyeuawa na mtu asiyejulikana aliyemkodi.
Ni huzuni kwenye msiba.
Mwananchi wa Kata hiyo akielezea tukio hilo kwa waandishi wa habari.
Ni huzuni katika msiba huo.




Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2