Mkuu wa wilaya ya Arumeru Eng.Richard Ruyango akiwa katika mafunzo ya siku mbili yaliyoanza leo tarehe 20/1/2020 ambayo ni ya kuwajengea uwezo wajasiriyamali ambao ni wazalishaji,wasindikizaji,na wauzaji wa bidhaa zitokanazo na maziwa
Afisa viwango Joseph Basil Tarimo -Kamati ya uandaaji wa viwango vya maziwa na bidhaa zake (TBS)akizungumza na wajasiriayamali ambao ni wazalishaji,wasindikaji na wasambazaji wa maziwa, bidhaa zigokanazo na maziwa,kuzingatia kanuni Bora za matakwa ya viwango.
Wajasiriayamali ambao ni wazalishaji,wasindikaji na wasambazaji wa maziwa, bidhaa zigokanazo na maziwa,wakifuatilia kwa makini mafunzo yanayoendelea yaliyoandaliwa na TBS namna ya kuzingatia kanuni Bora za matakwa ya viwango.
Afisa viwango Joseph Basil Tarimo akizungumza na wajasiriayamali ambao ni wazalishaji,wasindikaji na wasambazaji wa maziwa, bidhaa zigokanazo na maziwa,kuzingatia kanuni Bora za matakwa ya viwango.
Na.Vero Ignatus,Arusha
Takwimu za sensa ya mifugo na uvuvi mwaka 2019-2020 zinaonyesha kuwa uzalishaji wa maziwa ya ng'ombe nchini Tanzania ni lita bil 3.13 kwa mwaka, kati ya hizo lita bil 3.11 sawa na 96.4% zinazalishwa na wafugaji wadogo ,ambapo lita bil 17.8 sawa na 0.6%hutoka mashamba makubwa , hivyo kwa mujibu wa takwimu hizo zinadhihirisha kuwa wafugaji wadogo ni wengi kuliko wakubwa na ndio wanaozalisha malighafi kwa wingi
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Eng.Richard Ruyango katika Mafunzo ya siku mbili yanayoendelea Mkoani Arusha iliyoandaliwa na TBS, kwa wazalishaji,wasindikaji na wasambazaji wa maziwa, bidhaa zitokanazo na maziwa, na kuwataka kuzingatia kanuni Bora za matakwa ya viwango
Aidha Ruyango ametoa rai kwa wajasiriyamali hao, kutambua kuwa uzalishaji wa maziwa unahitajika kuwa bora,sambamba na kutambulika ubora wake kabla ya kupelekwa kwenye matumizi ya kinadamu, kwani itawasaidia kwa pamoja kuelewa uzalishaji unaokidhi viwango,ubora,na usalama ili kulinda Afya ya mlaji pamoja na kukuza uchumi wa taifa haswa katika suala la ushindani
Kwa upande wake Afisa Viwango kutoka Shirika la viwango Tanzania (TBS) Joseph Bazil Tarimo amewataka wajasiriayamali kutambua kuwa ,matakwa ya kuzingatia katika kiwango cha maziwa, ni pamoja na malighafi ya viungo vinavyohitajika ,uhalisia wa bidhaa husika,kikomo salama cha bakteria,kikomo salama cha vichafuzi ikiwemo sumu kuvu na madini tembo sambamba na vifungashio
Tarimo ameeleza kuwa Matakwa ya viwango hivyo ni pamoja na kuwa na namba maalum inayotofautisha kiwango kingine,ambapo namba ya viwango lazima ianze na TZS ,mfano kiwango cha maziwa ghafi (Raw cow milk-specification) ni Tzs 626 kilichochapishwa mwaka 2019, kama kiwango cha kitaifa .TZS 626:2019/EAS 67:2019, ambapo kinaeleza mahitaji na njia za majaribio ya kimaabara ya maziwa ghafi yanayozalishwa kwaajili ya matumizi ya binadamu .
Sambamba na hilo amewataka kutambua kuwa kikomo salama cha vijidudu kinachoruhusiwa katika maziwa ,yanatakiwa wasiwe na fangas wala bakteria zinazoweza kuleta madhara kwa mtumiaji
''Tambueni kuwa faida za viwango ni pamoja na kulinda Afya na Usalama wa walaji,kuweka Usalama katika uwanja wa biashara,huondoa mchanganyiko juu ya bidhaa,uhakikisho wa ubora,Usalama wa kuaminika na ufanisi''.Alisema Tarimo
Aliwakumbusha matakwa ya kuzingatia katika maziwa ( cow milk) yanatakiwa yawe na kiasi cha mafuta kisichopungua 3.25% kiasi cha protini kisichopungua 3% vitu ya bisi ambavyo siyo mafuta visipungue 8.5%,PH 6.6 -6.8,tindikali isizidi 0.17%,pamoja na wiani wa maziwa (destiny)g/ml katika 20 )0C iwe 1.028-1.032
Kwa upande wake mshirikiwa mafunzo hayo kutoka mfugaji na muuza maziwa Wilium Boaz Laizer kutka katika kijiji cha Lenjanitarafa ya Muklati ArushaDC :Mimi ni mfugaji anzia mwaka 1995 nilianza kufuga ng'ombe wa kisasa hadi sasa ninao 6na ndama 4,changamoto kubwa ninayopata ni malisho,nyakati za kiangazi tunapata tabu sana ,hivyo gharama ya maziwa ni kubwa kwani tunanunua majani.
Nategemea baada ya mafunzo hayo tutapata majibu ya changamoto hizo tufanyeje?kwani hapa darasani wapo watalaamu wengi, changamoto nyingine ni soko la maziwa haliaminiki,kukiwa na uhakika wa masoko hata gharama ikiwa kubwa tutakuwa na moyo wa kuendelea kufuga kwani soko lipo tu.Anasema Laizer
Naye mshiriki wa mafunzo hayo ambaye ni msindikaji wa maziwa kutoka (W)Siha mkoani Kilimanjaro Merry Mmary:wafugaji wakifuga ngombe kwa ubora watatuletea maziwa bora zaidi, kwani changamoto kubwa tunazokutana nazo ni pamoja na kutokupata maziwa bora
''Wafugaji hawa hawa wakikamua maziwa wanaongeza maji ,sasa wakati tunapopima sisi tunawarudishia! lakini kutokana na elimu hii ambayo TBS wanatoa haswa kwa wafugaji wataona umuhimu wa kutoa maziwa bora ili na sisi wasindikaji wa maziwa tuweze kupata maziwa bora''.Alisema Merry.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment