THAMANI YA MFUKO WA HIFADHI YA JAMII (NSSF,) YAZIDI KUPAA | Tarimo Blog


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati akizindua Bodi ya wadhamini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF,) na kuwataka wajumbe na uongozi kuendelea kushirikiana ili kuleta manufaa chanya zaidi, leo Mjini Morogoro.Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba akitoa maelezo ya utangulizi wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF,) leo mjini Morogoro.

Mwenyekiti Mpya wa Bodi, Balozi Ali Idi Siwa akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Bodi hiyo na kueleza kuwa wataendelea na kasi katika utendaji kazi ili kuleta maendeleo chanya kwa jamii, leo Mjini Morogoro.
Profesa Jamal, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Jamal Katundu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo, Mjini Morogoro.


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu; Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama amesema kuwa thamani ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF,) umepanda hadi kufikia shilingi Trilioni 5.4 kwa Takwimu za Desemba 2021.

Hayo ameyaeleza leo mjini Morogoro wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini na kueleza kuwa bodi hiyo kwa kushirikiana na uongozi wa mfuko huo wamekuwa wakishirikiana  katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kote nchini.

"Balozi Ali Idi Siwa Ali Mwenyekiti wa bodi hii ameteuliwa kwa kipindi cha pili zaidi cha miaka mitatu nimpongeze kwa kuaminiwa na Rais Samia Suluhu Hassan yeye na wajumbe wote, mkawe wasimamizi wazuri wa mfuko huu.....Mfuko huu sio mdogo hesabu za Desemba 2021 thamani yake imepanda hadi kufikia shilingi Trilioni 5.5, Kazi iendelee kwa kasi zaidi." Amesema.

Waziri Mhagama ameiagiza Bodi hiyo kufanya kazi kwa ustawi wa Mfuko kwa kuzingatia sheria pamoja na kupanua wigo wa uchangiaji kwa kuandikisha wanachama ili kuongeza thamani ya Mfuko huo.

Aidha amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa NSSF Masha Mshomba kwa kuwaweka pamoja wafanyakazi wa NSSF na kufanya shuguli za kimaendeleo kwa umoja na manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Vilevile amemwagiza Mkurugenzi huyo kuondoa nafasi za ukaimu kwa wakurugenzi waliokaimu kwa muda mrefu kwa kuwapa ukurugenzi kamili ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. 

Kwa upande wake Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wadhamini Balozi Ali Idi Siwa amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa uteuzi huo na kuahidi kufanya kazi kwa weledi na malengo kwa kushirikiana na wajumbe wote wa bodi na uongozi wa NSSF.

Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Masha Mshomba amesema, wakiwa kama Taasisi wana mipango ya utekelezaji pamoja na maelekezo yaliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan Bungeni.

"Tunakwenda kuvuka malengo na mikakati ya maendeleo tuliyoweka kufikia 2025 kupitia bodi hii ambayo ina uzoefu wa kutosha." Amesema.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martin Shegela, Naibu Katibu Mkuu, Ofisini ya Waziri Mkuu Prof. Jamal Katundu na Menejimenti ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF.)

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (wanne kushoto) akimkabidhi kitendea kazi, Katibu wa Bodi ya Wadhamini Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, (NSSF) ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo,  Bw. Masha Mshomba. ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa Bodi hiyo kweny ukumbi wa NSSF mjini Morogoro Januari 8, 2021. Wengine pichani ni Mwenyekti mpya wa Bodi hiyo, Balozi Ali Idi Siwa, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Martin Shigela, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa Jamal Katundu.





Wajumbe wa Bodi wakikabidhiwa vitendea kazi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (watatu kushoto) akimkabidhi kitendea kazi, Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Wadhamini, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, (NSSF), Balozi Ali Idi Siwa, ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa Bodi hiyo kwenye ukumbi wa NSSF mjini Morogoro Januari 8, 2021. Wanaoshuhudia kutoka kushoto, ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Martin Shigela, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa Jamal Katundu, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba.
Mkutano ukiendelea.






Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2