NA MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uratibu Mhe . Balozi Pindi Chana ameomba Wazee wa Mji wa Dodoma kuendelea kuishauri Serikali, katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Miradi ya Maendeleo zinazotekelezwa.
Hayo yamesemwa na Mhe. Balozi Chana alipokutana na Baraza la Wazee wa 22/01/2022 Mjini Dodoma waliotembelea kujionea ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba Mjini Dodoma. Ameeleza kwamba Ujenzi wa Mji wa serikali unahitaji bajeti yakutosha, Uongozi wa Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan umeonesha nia ya dhati ya kuleta mabadiliko ya kimaendeleo na kimapinduzi kwa kuhakikisha kwamba Taasisi za serikali zinahamia Dodoma kwa wakati unaostahili.
Aidha ujenzi wa miundo mbinu ya awali katika Mji wa Serikali Mtumba umekamilika, huku ujenzi wa Barabara za Mji wa Serikali Mtumba ukiwa umekamilika kwa 94%. Ameongeza kusema ujenzi wa miundo mbinu ya kudumu ya Maji Safi, Maji Taka, Umeme Mawasiliano, Tehama, Usalama Zimamoto na Upandaji wa Miti ipo katika hatua za mwisho ya kuanza utekelezaji wake.
Mhe. Balozi Chana ametoa rai kwa Wazee wa Mji wa Dodoma kuendelea kuishauri Serikali. “Wazee ni Mabalozi wazuri wa serikali kwa wananchi, nyinyi ndio wadau wakubwa kwa kuhakikisha serikali inahamia Dodoma” Amesema Mhe. Balozi Dkt. Chana. Ujenzi wa miundo mbinu mingi umeendelea chini ya uongozi wenu, tundelee kuunga mkono jitihada za serikali zinazoongozwa chini ya uongozi wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha Uchumi wa Nchi na kulinda Amani ya Nchi kwa maendeleo yetu.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mjini Dodoma Mhe. Peter Mavunde amesema wanafuraha kubwa ya kuruhusiwa kutembelea Mji wa Serikali Mtumba. Mji wa Serikali una historia ndefu, kutangazwa kuhamishwa kwa Mji wa Serikali Kulitangazwa na Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere, na dhamira ya kuhamisha Makao Makuu kuja Dodoma ikaendelea kuwepo katika Awamu zote za uongozi.
Ameeleza katika kuadhimisha miaka 60 ya uhuru, Serikali ya Awamu ya sita Inayoongozwa na Rais Mhe, Samia Suluhu Hassani iliweka Mawe ya Msingi Katika wizara zetu ikiwa ni ishara ya kuwa makao ya kudumu katika Mji wa Serikali Mtumba. Amesema jambo hilo limewafurahisha Wazee wa Mji wa Dodoma na kuwahamasisha kutembelea, kujionea na kujifunza kuhusu ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba Dodoma.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Dodoma Mjini Meja Mstaafu Johnick Risasi amesema ili amani iwepo, kila mmoja wetu anapaswa kuitunza kwa sababu ni tunu. Amefafanunua ili tuweze kuitunza, kila mtu anayeshika Madaraka katika nyadhifa mbalimbali lazima awe na upendo, unyenyekevu, na kuheshimu watu. Wazee tuna jukumu la kuelimisha vijana ili kuwapa urithi mzuri wa baadae.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (sera Bunge na Uratibu) Mhe. Balozi Pindi Chana akisisitiza jambo alipokutana na Baraza la wazee Mji wa Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu ) Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akizungumza na Baraza la Wazee Mjini Dodoma, waliokuwa katika ziara ya kutembelea Ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba.
Wazee wa Mji wa Dodoma wakipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu kwenye Mradi wa Ujenzi wa Hoteli inayojengwa na Jiji la Dodoma .
Matukio katika picha Wazee wa mji wa Dodoma wakimsiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana alipokutana na Baraza la wazee hao Mji wa serikali Mtumba
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment