AMREF AFRICA WAZINDUA MIRADI MIWILI YA WAWE NA WADA II MKOANI IRINGA | Tarimo Blog

Meneja wa Mradi wa Amref Health Africa, Eng. James Mturi akiongea wakati wa uzinduzi wa miradi miwili mkoani Iringa.
Picha ya pamoja ya viongozi wa serikali ya mkoa wa Iringa na baadhi ya wafanyakazi wa AMREF ambao watakuwa wanatekeleza miradi yote miwili kwenye mikoa husika.
kaimu RAS wa mkoa wa Iringa anayeshughulikia maswala ya serikali za mtaa Wilfredy Myuyu aliwapongeza Shirika la Amref Health Africa kwa kuzindua miradi miwili ambayo itasaidia kuchochea maendeleo kwa wananchi wa mkoa wa Iringa.
Baadhi ya washiriki wa uzinduzi wa miradi miwili inayotekelezwa na AMREF AFRICA

Na Fredy Mgunda,Iringa.
SHIRIKA la Amref Health Africa lazindua mradi wa usafi wa mazingira na uwezeshaji wanawake (WAWE) na Mradi wa Maji na Maendeleo (WADA II) mkoani Iringa kwa lengo la kuboresha afya na ustawi wa kiuchumi wa wanawake na vijana Pamoja na upatikanaji wa huduma za maji na usafi wa mazingira katika jamii, shule na vituo vya afya.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa miradi hiyo miwili Meneja wa Mradi wa Amref Health Africa, Eng. James Mturi alisema kuwa mradi wa Maji na Maendeleo (WADA II) utatekelezwa katika vijiji tisa (9) kwenye mikoa mitatu ambapo Mkoa wa Iringa vitanufaika vijiji saba, Mkoa wa Njombe kijiji kimoja na mkoa wa Morogoro kiji kimoja.

Alisema kuwa Vijiji vitakavyonufaika na huu mradi ni Nyabula,Mlanda,Ndiwili,Mkungugu, Nyang’oro and Makwawa katika mkoa wa Iringa, Magogoni mkoani Morogoro na Wanginyi mkoa wa Njombe na mradi utahusisha, uchimbaji wa visima vipya vitatu kwenye vijiji vitatu, ujenzi wa vyoo kwenye shule tano, ukarabati wa vyoo na miundo mbinu ya maji kwenye shule tano na vitua vya kutolea afya tisa.

Mturi alisema kuwa mradi mpya unalenga kuboresha afya na hali ya kijamii na kiuchumi, kwa jamii lengwa hususan wanawake na vijana kwa kuboresha upatikanaji wa huduma za maji na usafi wa mazingira katika jamii, shule na vituo vya afya.

Alisema kuwa Mradi wa ‘Maji na maendeleo (WADA)’ utakaotekelezwa katika mikoa mitatu unaunga mkono juhudi na malengo ya wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA), kwa kutoa huduma ya majisafi, salama na usafi wa mazingira vijijini kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Mturi alisema kuwa lengo la mradi ni Kuongeza upatikanaji wa maji kwa kupitia miundo mbinu inayotumia umeme jua,Kuboresha miundo mbinu itakayoongeza usafi wa mazingira kwenye shule na vituo vya afya,Kutathimi uwezo wa RUWASA kwenye kuendeleza miradi ya maji na usafi wa mazingira,Kutathimini na kujaribu kutafuta utatuzi wa athari ya mabadiliko ya tabia ya inch kwenye miundo mbinu yam aji na usafi wa mazingira.

Alisema kuwa Mradi huo umepewa jina la ‘Mradi wa Maji na Maendeleo (WADA) ni mradi wa mwaka mmoja unaofadhiliwa na shirika la msaada la watu wa marekani (USAID) na Cocacola, na utatekelezwa kwa ushirikiano na worldserve international, na kupata miongozo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na wizara ya elemu sayansi na teknolojia.

Aidha Mturi alisema kuwa katika Mradi wa usafi wa mazingira na uwezewshaji wanawake katika Halmashauri za wilaya ya Kilolo na Mufindi mkoani Iringa yaani WASH and Women Empowerment project (WAWE) utakaotekelezwa katika jamiii zinazolima chai na kahawa katika Halmashauri za wilaya ya Kilolo na Mufindi. Mradi huu wa mwaka mmoja unafadhiliwa na Starbucks Foundation na kutekelezwa na shirika la Amref Health Africa

Mturi alisema kuwa Mradi huu unalenga kuboresha afya na ustawi wa kiuchumi wa wanawake na vijana 184,500 katika jamii zinazolima kahawa na chai katika wilaya za Kilolo na Mufindi.Utekelezaji wa mradi huu utaondoa vikwazo vya elimu, afya bora, lishe endelevu na usafi wa vyoo na maji salama.

Alisema kuwa lengo la mradi ni Kuanzisha vikundi vya ujasiriamali kwa vijana na wanawake katika jamii zinazolima kahawa na chai katika Halmashauri za wilaya za Mufindi na Kilolo,Kuhamasisha upatikanaji wa maji salama, vyoo bora na usafi wa mazingira katika jamii zinazolima kahawa na chai katika Halmashauri za wilaya za Mufindi na Kilolo,Kuwezesha wanawake na vijana katika ukuaji wa kiuchumi katika Halmashauri za wilaya za Mufindi na Kilolo.

Mturi alisema kuwa mradi huo unasimamiwa na shirika la Amref Health Africa kwa kushirikiana na Halmashauri za wilaya ya Kilolo na Mufindi pamoja na idara nyingine za serikali katika ngazi ya mkoa na taifa.

Kwa upande wake kaimu RAS wa mkoa wa Iringa anayeshughulikia maswala ya serikali za mtaa Wilfredy Myuyu aliwapongeza Shirika la Amref Health Africa kwa kuzindua miradi miwili ambayo itasaidia kuchochea maendeleo kwa wananchi wa mkoa wa Iringa.

Myuyu alisema kuwa miradi hiyo ikikamilika inatakiwa kutunzwa kwa ngazi zote kwa kuwa itakuwa inasaidia kuboresha afya,kukuza uchumi na kuleta maendeleo kwa wananchi ambao wananufaika na miradi hiyo.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2