Baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Busega limepitisha bajeti ya jumla ya Tsh 32,397,778,860 kwaajili ya mwaka wa fedha 2022/2023. Baraza hilo ambalo limefanyika tarehe 23/02/2022, ambapo wajumbe wa baraza hilo wameridhishwa na vile bajeti hiyo ilivyotayarishwa.
Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Busega Mhe. Sundi Muniwe amesema anaamini bajeti hiyo ambayo imepitishwa kwaajili ya utekelezaji wake kwa mwaka ujao wa fedha, itakidhi matakwa ya Halmashauri kwakuwa imekuwa bajeti iliyoelekezwa zaidi kwenye vipaumbele vya Halmashauri. “Tuna imani kubwa na bajeti hii kwa maana imeandaliwa vyema tofauti na baadhi ya bajeti za miaka iliyopita, hivyo ikitekelezwa katika uhalisia wake tutafikia malengo ya vipaumbele tulivyojiwekea”, alioneza Muniwe.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Veronica Sayore amesema kwamba utekelezaji wa bajeti unategemea na upatikanaji wa fedha, na anamini bila shaka bajeti iliyopitishwa na baraza la madiwani itasimamiwa vyema ili kutekeleza yale yote yaliyopendekezwa. “Tutasimamia vyema utekelezaji wa bajeti iliyopitisha, ili kuhakikisha vipaumbele vilivyobainishwa ikiweo miradi ya maendeleo inatekelezwa”, alisema Sayore.
Aidha, Sayore amesema, miradi mbalimbali na vipaumbele vilivyobainishwa itatekelezwa kwa wakati kwa kusimamia vyema mapato ya ndani ili kutekekleza miradi mbalimbali inayotokana na fedha za mapato ya ndani. “Tutaimarisha vikosi kazi, na mbinu mpya zitakazoongeza mapato ya Halmashauri kwa kiasi kikubwa ili kuwezesha utekelezaji wa bajeti hii”, aliongeza Sayore.
Madiwani wanasema bajeti hii ina maono mazuri kwani imeainisha maeneo muhimu ambayo yataleta chachu kubwa ya Maendeleo kwa Wilaya ya Busega. Miongoni mwa vipaumbele vilivyobainishwa ni pamoja na utengenezaji wa miundombinu katika taasisi zikiwemo shule, Zahanati na vituo vya afya. Maeneo mengine ni pamoja ya kuimarisha ustawi wa jamii kwa kutoa Mikopo ya asilimia 10 na kusimaia vyema fedha za mpango wa kunusuru kaya masikini (TASAF).
Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Busega kwa mwaka wa fedha 2022/2023 imepitishwa na baraza la madiwani, ikiwa imetokana na vyanzo vitatu, ikiwemo ruzuku kutoka Serikali kuu ikiwa ni Tsh 23,859,949,340 sawa na asilimia 73.6, fedha za wahisani Tsh 5,769,585,720 sawa na asilimia 17.8 na vyanzo vya mapato ya ndani Tsh 2,768,243,800 sawa na asilimi 8.5.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment