DC MOYO ATAKA ELIMU YA UKATILI WA KIJINSIA ITOLEWE MARA KWA MARA IRINGA | Tarimo Blog


Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akisisitiza jambo kuhusu ukatili wa kijinsia (picha kutoka maktaba)




Na Fredy Mgunda,Iringa


UELEWA hafifu walio nao baadhi ya wataalam wa afya juu ya ujazaji wa fomu za matibabu PF3 zinazohusu kesi za ukatili wa kijinsia umetajwa kuwa ni Kikwazo katika kufanikisha ushahidi sahihi unaoweza kumtia hatiani mshtakiwa

Mwezeshaji katika Warsha ya kushughulikia mashauri ya wahanga wa ukatili wa kijinsia Mkemia Lutengano Mwanginde alisema kesi nyingi uharibika kwa kukosa ushahidi kwa fomu hizo kutojazwa vizuri, hali inayosababisha haki kupotea

Awali akizindua Warsha hiyo ya siku tatu Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo Amezitaka mamlaka zinazoshughulikia kesi za wahanga wa ukatili kufanyakazi kwa weledi na ushirikiano ili kukomesha ukatili unaoendelea

Moyo alisema kuwa chimbuko la masuala ya ulinzi na usalama wa wanawake na Watoto ni mikataba mbalimbali ya umoja wa mataifa kama vile (the united national convention on the rights of the child,November 1989 article 19) ikizielekeza nchi zote wananchama kuchukua hatua zote Madhubuti za kisheria,kiutawala,kijamii na kieleimu ili kulinda Watoto dhidi ya vitendo vya ukatili.

Alisema Watoto wa kike watatu kati ya kumi na wakiume mmoja kati ya saba wakiwa chini ya umri wa miaka 18 wanaripotiwa kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kingono.

Moyo alisema kuwa asilimia 72 ya Watoto wa kike na asilimia 71 ya Watoto wa kiume wakiwa chini ya umri wa miaka 18 wanalipotiwa kufanyiwa ukatili wa kimwili na asilimia 60 ya waliolipotiwa wanafanyiwa na wazazi na asilimia 50 ya walioripotiwa walifanyiwa na walimu.

Alisema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha linapunguza matukio ya ukatili kwa asilimia 50 ifikapo juni 2022 hivyo kupitia mafunzo hayo kwa wataalam wa ngazi mbalimbali Manispaa ya Iringa watapunguza vitendo hivyo kwa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi na wadau mbalimbali.

Moyo alisema kuwa anamatumaini makubwa kuwa watu wote waliopata mafunzo hayo watakuwa mabalozi wazuri kwa wafanyakazi wenzao na jamii kwa ujumla namna ya kupinga ukatili kwa jamii husika.

Warsha hiyo ya siku tatu imezinduliwa na mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo na alisema utafiti wa mwaka 2011 uliofanywa na Wizara ya afya kwa kushirikiana na Shirika la kuhudumia watoto UNICEF ulibaini hali mbaya ya ukatili hasa dhidi ya watoto

Alisema utafiti huo umeisaidia serikali kuandaa mpango wa ulinzi na usalama wa mtoto uliojikita katika kukabiliana na vitendo hivyo na kupunguza vitendo vya ukatili kwa asilimia 50 ifikapo mwezi june mwaka huu.

Mohamed Moyo alisema kupitia mafunzo hayo anatarajia kuona kasi ya kupungua kwa vitendo vya ukatili iliwa ni pamoja na kuchukuliwa hatua dhidi ya wote wanaohusika.

Faith Dewsi ni miongoni mwa wawezeshaji katika warsha hii juu ya masuala ya utetezi wa haki za watoto alisema utoajia wa taarifa katika ngazi ya afya ni miongoni mwa changamoto inayokwamisha vita ya mapambano ya ukatili dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Dewsi alisema kwa asilimia kubwa wanaoongoza kwa kufanyiwa ukatili wa kijinsia ni wanawake na Watoto hivyo jamii inatakiwa kupewa elimu mara kwa mara ili kuondokana na tabia hiyo.

Alisema mara nyingi ukatili ambao unatokea mara kwa mara ni Pamoja na ukatili wa kiuchumi,kimila,kisaikolojia na kingono hasa kwa wanawake ndio wanaongoza kufanyiwa ukatili.

Lutengano Mwanginde ambaye ni muwezeshaji mtaalam wa maabara alisema kuwa kuna changamoto kwa baadhi ya wataalam wa afya juu ya ujazaji wa fomu namba 3 ya polisi inayotumika kama ushahidi pindi mtuhumiwa wa ukatili anapofikishwa mahakamani.

Mwanginde kupitia warsha hiyo aliwakumbusha wataalam wa afya kuzingatia uchukuaji wa sampuri za vina saba ili kusaidia mahakama kujiridhisha na kutoa hukumu sahihi kwa mshtakiwa

Mwezeshaji huo alisema iko haja ya kuwapo kwa mafunzo ya mara kwa mara kwa wataalam wa afya ili kuwawezesha kutenda kazi yao kwa weledi la kuwa sehemu kusaidia kukomesha vitendo vya ukatili.

Warsha hii inayowakutanisha Wawakilishi kutoka idara za afya, mahakama, polisi na wadau wengine wa kupinga vitendo vya ukatili imejikita katika kujenga uelewa wa pamoja wa namna ya kushughulikia kesi zinazohusu ukatili kwa lengo la kupunguza ama kukomesha vitendo hivyo vya ukatili wa dhidi ya wanawake na watoto vinavyotajwa kushamiri katika maeneo ya Iringa


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2