MJUMBE WA BODI YA AGRA NA RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AISHAURI SERIKALI KUIMARISHA USHIRIKA | Tarimo Blog

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mh Dr.Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Shirika la  Mageuzi ya Kijani Afrika-AGRA ameishauri Serikali kuimarisha Vyama vya Ushirika ile viwe suluhisho ya upatikanaji wa masoko ya mazao ya wakulima.


Mh Kikwete ameyasema hayo leo tarehe 17 Februari, 2022 Wilaya za Mpanda na Tanganyika mkoani Katavi ambapo yupo ziara ya kikazi ya kutembelea wanufaika mbalimbali wa miradi inayotekelezwa chini ya ufadhili wa  AGRA.

"Hapo nyuma wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne, tuliamua kubeba madeni yote ya vyama vya ushirika ili kuweza kuviimarisha na kuviongeza nguvu ya kukopa na kuhudumia wakulima.

Miaka ya nyuma Serikali ilibaini kuwa viongozi wengi wa vyama vya ushirika walikuwa si waaminifu, hali iliyopelekea kuwepo kwa ubadhirifu mkubwa wa fedha za wakulima na mali za ushirika

Kimsingi, Serikali iliamua kuimarisha ushirika ili utumike kama nyenzo kuu ya kutafuta masoko ya mazao ya wakulima na kuwasaidia kupata pembejeo sahihi kwa wakati na kwa bei nafuu, hivyo Mhe. Mavunde, kama Serikali jaribuni kuimarisha ushirika ili uweze kusaidia kutafuta masoko ya mazao ya wakulima" alisema Mh Kikwete

Naye Naibu Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Mh Anthony Mavunde alieleza kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha ushirika ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025 na maelekezo ya Mheshimwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa tujenge ushirika imara, wenye nguvu na utakaomnufaisha mkulima na serikali kupitia Mrajis wa Ushirika itaendelea kuwachukualia hatua kwa mujibu wa sheria viongozi wote wa Ushirika watakaoshindwa kusimamia ushirika kwa mujibu wa sheria na kwa wale pia watakaobainika kufanya ubadhirifu.

 





Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2