Mnec Katavi apigwa msasa wa uongozi chuo Cha Mwalimu Nyerere | Tarimo Blog


Na Victor Masangu,Pwani.

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha mapinduzi (CCM) Taifa kutokea Mkoa wa Katavi Gilbert Sampa amesema kwa kujengwa kwa mradi mkubwa wa ujenzi wa chuo cha uongozi wa siasa cha Mwalimu Julias Nyerere kutaweza kuwa mkombozi mkubwa katika suala zima kujifunza uongozi.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa halfa ya ufunguzi rasmi wa chuo hicho ambacho kumefunguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa Chama pamoja na viongozi wa serikali wakiwemo viongozi wastaafu na mawaziri.

Mjumbe huyo ambaye naye alikuwa ni moja ya kiongozi ambao waliweza kuhitimu kozi ya muda mfupi katika Chuo hicho kwa kipindi cha muda wa siku sita na kufanikiwa kutunikiwa chetu.

"Tulikuwa viongozi mbali mbali zaidi ya 30 wakiwemo baadhi ya wakuu wa mikoa na tumepata elimu hii na kuweza kujifunza juu ya kuwa wazalendo na nchi,mambo ya maadili,pamoja na suala zima la itifaki mbali mbali kwa hivyo kwangu mm ni fursa ya kipekee ambayo itanisidia katika uongozi wangu,"alifafanua "Sampa

Mjumbe huyo kutoka Katavi aliongeza kuwa ujenzi wa shule hiyo itaongeza zaidi ushiriki wa pamoja baina ya Chama cha mapinduzi na vyama sita vya ukombozi vilivyopo kusini mwa bara la afrika ambavyo vimeweza kuleta mapinduzi makubwa katika kupambania suala zima la ukombozi.

"Tulikuwa viongozi mbali mbali zaidi ya 30 wakiwemo baadhi ya wakuu wa mikoa na tumepata elimu hii juu ya kuwa wazalendo na nchi,mambo ya maadili,pamoja na suala zima la itifaki mbali mbali kwa hivyo kwangu mm ni fursa ya kipekee ambayo itanisidia katika uongozi wangu,"aliongeza Gilbert.

Aidha alibainisha kwamba mafunzo hayo aliyoyapata yataweza kumsaidia kwa kiasi kikubwa katika suala zima la utekelezaji wa majukumu yake ya uongozi na kwamba atayatumia kwa maslahi ya Taifa kwa ujumla.

"Kimsingi mm ni mtu wa mwanzo kabisa kwa muhitimu ambao nimepata fursa ya kuhitimu mafunzo ya uongozi wa siasa kwa kweli katika siku hizi sita tumejifunza mambo mengi katika chuo hiki cha uongozi Cha Mwalimu Julias Nyerere kilichopo Wilayani Kibaha," alibainisha.

Katika hatua nyingine ambayo alisema kwamba atayavalia njuga ni kuhusiana na suala la kuwa mzalendo na nchi yake pamoja na masuala mbali mbali yanayohusiana na utekelezaji wa majukumu ya uongozi.

 


Caption-Mjumbe wa halmashau kuu ya CCM Taifa kutoka Mkoa wa Katavi Gilbert Sampa akizungumza kuhusiana na waandishi wa habari hawapo pichani.

 


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2