Na Khadija Kalili, Pwani
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua Chuo Cha Siasa Cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kibaha Kwa Mfipa Mkoani Pwani uzinduzi umepangwa kufanyika Februari 23 jumatano mwaka huu.
Akizungumza leo katika mkutano na Waandishi wa habari wa Mkoa wa Pwani Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge alisema kuwa hali ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa iko vizuri huku akitanabaisha kuwa wakaazi wa Mkoa huu wajitokeze kwa wingi Ili kutoa hamasa ya uzinduzi huo.
"Nimewaita ili niueleze umma kwa kupitia ninyi kuwa Mheshimiwa Rais wetu wa awamu ya sita Mama Samia Suluhu Hassan atafanya zaiara Maalumu katika Mkoa wa Pwani ambapo atakuja mahsusi kwa kufanya uzinduzi wa Chuo hiko ambacho kinamilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) pia ikiwa na vyama vyote vingine vya siasa barani Afrika ambavyo vilikuwa katika mstari wa
mbele wa ukombozi wa nchi zao alisema RC Kunenge.
RC. Kunenge aliongeza kwa kusema kuwa "wakaazi wa Mkoa wa Pwani tumepata heshima hivyo tujitokeze kwa wingi kuja kumlaki Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan " alisema .
Awali RC Kunenge alisema kuwa Februari 22 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo kwa kushirikiana na Makatibu Wakuu wanne wenzake kutoka katika vyama vingine ambavyo vilipigania uhuru wa nchi zao huku majina na nchi zake kwenye mabano ni ANC (Afrika ya Kusini) FRELIMO (Msumbiji) , SWAPO (Namibia) na ZANU PF ( Zimbabwe) , NPLA (Angola) wote kwa pamoja watazindua barabara yenye urefu wa Kilometa mbili inayokwenda chuoni hapo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment