Na Farida Said,Michuzi tv.
Watafiti na wataalamu wa kilimo hapa nchini wamewataka wakulima kuwa na tabia ya kupima udongo kabla ya kulima ili kutambua aina gani ya virutubisho vinavyokosekana pia kujua aina gani ya mazao yanatakiwa kulimwa kutokana na aina ya udongo hii itasaidia kuongeza kuzarishaji kwa wakulima hapa nchini.
Hayo wanajili baada ya Kituo cha Utafiti wa Kilimo nchini TARI UYOELE kufanya tafiti juu ya hali ya udongo unaotumiwa na wakulima wa Mikoa minne ya Rukwa,Morogoro, Iringa pamoja na Mbeya, ambapo kituo kimebaini udongo unaotumiwa na wakulima wengi wa mikoa hiyo umekosa rutuba hali inayosababisha wakulima kuendelea kukosa mazao yenye tija.
Akizungumza Mjini Morogoro baada ya kutoa taarifa ya Tafiti zilizofanyika katikaWilaya nane za Mkoa wa Morogoro Mkurugenzi wa kituo cha Utafiti wa Kilimo nchini TARI UYOLE Dkt. Tulole Bucheyeki amesema katika Mkoa huo kituo kimepima udongo na kubaini upungufu wa virutubisho vya Nitrogen, Sapha, Bollon na Zinki katika udongo hali inayosababisha wakulima kufanya kilimo cha mazoea na kukosa mavuno yenye tija.
Dkt. Bucheyeki amesema licha ya Mkoa wa Morogoro ya kuwa tegemezi katika mazao ya chakula na biashara lakini unakabiliwa na unaupungufu wa Virutubisho mbalimbali, ambapo kukosekana kwa kwa virutubisho hivyo katika udongo kunasabaisha wakulima kukosa mavuno yenye tija licha ya wakulima kutumia mbolea.
Ameongeza kuwa kukosekana kwa virutubisho katika katika udogo hakuathiri tu ukuaji wa mimea pia, unathiri hata ukuaji wa binaadamu, kutokana na kula chakula ambacho hakuna virutubisho sahihi kutoka kwenye nafaka na matunda.
Mratibu wa upimaji wa udongo kutoka kituo cha utafiti TARI UYOLE Bwana Fredrick Mlowe amewataka wakulima kuacha tabia ya kutumia mbolea kwa mazoea badala yake kutumia mbolea kwa kufuata ushauri wa wataalam wa kilimo kwani matumizi holela ya mbolea husababisha udongo kukosa virutubisho vinavyotakiwa.
“Tunalima miwa inakuwa mifupi kinachofanya miwa iwe mirefu na uvune kiasi kikubwa ni Zinki ambayo haipo kwenye mbolea nyingi ambazo tumezoea kuzitumia .” Alisema Bwana Mlowe.
Kwa upande wake Meneja wa OCT Tanzania Dkt Mshindo Msolla amesema changamoto kubwa inayowakumba wakulima wengi hapa nchini ni kukosa taarifa rasmi za afya ya udongo hali inayopelekea wakulima kufanya kilimo cha mazoea ambacho kinamnyima mkulima kupata mavuno yenye tija.
Aidha ameiomba Serikali kuongeza tija kwenye mazao ya mkulima kwa kusimamia vinzuri matumizi bora ya mbegu, mbolea pamoja na upimaji wa udongo kwa wakulima wakubwa na wadogo hapa nchini.
Nae Kaimu Mkurugenzi idara ya mipango na matumizi bora ya ardhi kutoka Wizara ya Kilimo Eng.Juma Mdeka amesema zaidi ya wakulima Elfu tatu na mia tano (3500) wamepatiwa elimu juu ya matumizi sahihi ya mbolea na upimaji wa odongo.
Zoezi la upimaji wa udongo limefanyika katika mikoa nane ya Rukwa, Iringa, Mbeya pamoja na Morogoro ambapo kwa Mkoa wa Morogoro Maafisa ugani 34 wamepatiwa mafunzo pamoja na vijiji 100 kupima upimwa udongo.
Mratibu wa upimaji wa udongo kutoka kituo cha utafiti TARI UYOLE Bwana Fredrick Mlowe akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutoa hitisho ya tafiti zilizofanywa katika Mkoa wa Morogoro juu ya upimaji wa udongo na matumizi bora ya mbelea February 14.2022.
Mratibu wa upimaji wa udongo kutoka kituo cha utafiti TARI UYOLE Bwana Fredrick Mlowe akitoa wasilisho kwa wataalamu wa kilimo Mkoa wa Morogoro February 14.2022.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment