Na Amiri Kilagalila,Ruvuma
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mahanje halmashauri ya wilaya ya Madaba mkoani Ruvuma wamemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuunda tume maalum ikachunguze mgogolo uliopo baina yao na mamlaka ya bonde la ziwa Nyasa.
Wakazi hawa ambao ni wakulima wa mazao mbali mbali ikiwemo Mahindi,Maharagwe,Ndizi na mazao mengi mchanganyiko wanasema mgogolo wao mkubwa na mamlaka hiyo ni kutokana na kuzuiwa kuingia na kuendeleza kilimo katika eneo la zaidi ya ekari 400 walilokuwa wakilitumia miaka yote ikidaiwa kuwa ni sehemu ya hifadhi ya vyanzo vya maji Namahove.
Wakazi hawa akiwemo Christian Ngonyani,Joseph Chipeta na Joyce Mvula wanasema kwa sasa wamekuwa ni wahanga wakubwa katika maeneo yao hali inayowasababishia balaa la njaa kutokana na kukosa maeneo ya kulima.
“Nimenyang’anywa maeneo katika eneo la kibandisi mpaka sasa hatuna eneo la kulima,tunashinda njaa na maisha yamekuwa ni magumu tunaomba mama Samia utusaidie kwa kuwa tumewekewa vibao na kuambiwa ni marufuku kuingia kwenye eneo hili”alisema Joyce Mvula
Joyce Chipeta alisema “Kutoka kwenye mlima kule mpaka hapa tulipo ni zaidi ya kilomita mbili ambako ndipo yalipo mashamba ya watu na kitendo kilichofanyika hakijafanyikia kwa uhalali kwasababu haujafanyika ushirikishwaji”
Diwani wa kata ya Mahanje bwana Stephano Mahundi anasema baadhi ya mikutano ilifanyika ili kutoa elimu kwa wananchi juu ya mchakato uliofanyika lakini wananchi wa kijiji hicho wameona wameona utaratibu uliofanyika haukuwa sawa.
“Kwa Mahanje watu walifikiri kauli ile ya mita 60 ndio maeneo ambayo yatachukuliwa lakini kilichotokea sasa baada ya kuweka mipaka wananchi wameona ni tofauti na kile ambacho walifikiri”alisema Mahundi
Bi,Elice Engelbert ni mkurugenzi wa bodi ya bonde la ziwa Nyasa,amekili juu ya kuweka mipaka hiyo huku akibainisha kuwa vikao kadhaa na wananchi vimefanyika juu utunzaji wa eneo hilo mpaka kuweka mipaka huku akishangazwa na malalamiko ya wananchi hao na kuongeza kuwa eneo hilo limekuwa na migogoro pia ya mipaka.
“Watanzania wanajua chanzo cha maji ni pale maji yanapotokea tu,sio hivyo tu ila ni kuanzia pale ambapo maji yanatoka,yanatiririka mapaka yanapoishia.lakini sasa unaweza kukuta maeneo mengi ambayo mito mingi inaingia haya maeneo hayawezi kuwa sawa na utakuta kuna maeneo bikoni imekaa mbali na sehemu nyingine imeingia ndani kutokana na kipimo”alisema Bi,Elice
“Sheria ya mazingira inasema mita 60 lakini kuna sheria ya rasilimali za maji inakwenda zaidi ya mita 60 kwa eneo ambalo ni la maji na umuhimu wa hicho chanzo na hicho ndicho kipaumbele kwa hiyo eneo la chnazo linakwenda zaidi ya hapo na tulichokifanya Mahanje bado hatujachukua maeneo yote”aliongeza
Aidha Bi,Elice Engelbert amesema msimamo wa bodi ya maji bonde la ziwa Nyasa ni kuendelea kusimamia kikamilifu eneo hilo na kuagiza wananchi kutoingilia maamuzi juu ya eneo hilo na wapo tayari kuchukua hatua ya kisheria kwa mwananchi atakayekaidi maelekezo ya bodi kwa kuwa walikwisha toa maelekezo.
bango kubwa la ilani na muonekano wa bikoni zilizowekwa na bodi ya bonde la ziwa Nyasa katika maeneo ya Mahanje likielekeza kuto kuingia katika maeneo hayo kwa kuwa ni ya hifadhi
Baadhi ya wakazi wa Mahanje wakieleza masikitiko yao juu ya kupokwa ardhi yao inayokadiriwa kufikia ekari 400 na kuwasababishia kukosa maeneo ya kilimo. Shamba la matunda la Parachichi lililopo ndani ya eneo lililozuiwa kuendelea shughuli za kilimo. Moja ya eneo ambalo limeachwa kulimwa kutokana na katazo Wananchi wakionyesha maeneo yao ambayo wamezuiwa na mamlaka ya bonde kuendelea na shughuli mbali mbali.
Mama akichuma mboga katika shamba lake aliloacha kulima kutokana na zuio la kuendelea kulima kwenye maeneo hayo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment