Na Mwandishi Wetu
Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetembelea kiwanda cha bia cha Kampuni ya Serengeti (SBL) cha Dar es Salaam na kuelezea kuridhishwa na uwekezaji inayofanya kampuni hiyo hapa nchini.
Akiongea katika ziara hiyo iliyolenga kuangalia namna zoezi la utekelezaji wa stempu za kielekroniki unavyoendelea, mwenyekiti wa bodi hiyo Ulledi Mussa alisema uwekezaji unafanywa na SBL unatija kubwa kwa taifa.
“Upanuzi mkubwa wa viwanda vyenu unaonyesha kuwa mpo na mtanendelea kuwepo. Serikali ipo Nyuma yenu na changamoto mbali mbali za kikodi zzitakuwa zikendelea kufanyiwa kazi ili kuwawekea mazingira mazuri zaidi ya kufanya kazi,” alisema
Mwenyekiti huyo alisema kuwa TRA inaichukulia kampuni ya SBL km mdau muhimu wa maendeleo na kushukuru kwa uwekezaji wake katika miradi mbali mbali ya kijamii.
Kwa upande wake, mkurugenzi wa mahusiano kwa umma wa SBL John Wanyancha alisema kampuni hiyo imekuwa ikiwekeza katika midari mbali mbali ya kijamii kama vile maji, elimu, Kilimo endelevu na nyinginezo.
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Bia ya SBL Mark Ocitti (kushoto) akiongea na wajumbe wa bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) muda mfupi kabla ya ziara ya kutembelea kiwanda cha SBL Dar es Salaam kuangalia namnamfumo wa stempu za kielekroniki unavyofanya kazi.
Meneja wa kiwanda cha bia cha SBL Dar es Salaam Shekar Masakare akiwaonyesha wajumbe wa bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) namna mfumo wa stempu za kielekroniki unavyofanya kazi wakati wa ziara yao ya kutembelea kiwanda.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment