CHUO CHA UHASIBU ARUSHA WAKISHIRIKIANA NA TAKUKURU WAFANYA SEMINA KWA WAFANYAKAZI | Tarimo Blog
Na Pamela Mollel,Arusha
Chuo cha Uhasibu Arusha kwa kushirikiana na Taasisi ya kupambana na Rushwa(Takukuru)Mkoa wa Arusha imeendesha semina ya maadili kwa wafanyakazi na wahadhiri Chuoni hapo kutambua namna bora ya kupambana na Rushwa
Akizungumza katika semina hiyo Afisa uchunguzi kutoka Takukuru Salum Nyangwese ambaye alikuwa mtoa mada alisema kuwa mazingira ya rushwa hutengenezwa na wafanyakazi wasio na maadili kazini
Kwa upande wake mwanasheria wa Takukuru Violet Machery amewataka wafanyakazi hao kuzingatia mafunzo hayo ili kufanya kazi kwa weledi na umakini katika utekelezaji wa majukumu yao
Wanufaika wa semina hiyo walishukuru kwa uwepo wa mafunzo hayo ambayo yatawajengea uwezo na uelewa mkubwa katika kutambua vitendo vya rushwa
Lengo la semina hiyo ni kuboresha utendaji kazi pamoja na watumishi kufata maadili ya utumishi wa Umma.
Mwanasheria wa Takukuru Violet Machery akitoa mada katika Chuo cha uhasibu Arusha.
Afisa Uchunguzi kutoka Takukuru Mkoa wa Arusha Salum Nyangwese akitoa mada
Wafanyakazi wa uhasibu Arusha wakifatilia mada mbalimbali
Mwanasheria wa Takukuru Violet Machery akitoa mada katika Chuo cha uhasibu Arusha
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment