Kutokana na mgao wa maji uliokuwepo kwa wakazi wa Chalinze, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) sasa imehitimisha changamoto hiyo ya muda mrefu ya maji.
Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa maji wa Mlandizi - Chalinze - Mboga Mwenyekiti wa Bodi Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange amesema kuwa wakati umefika kwa wakazi wa Chalinze na maeneo ya karibu kupata majisafi kwani mradi huo umekamilika hivyo amewataka wananchi kwenda kwenye ofisi za Mamlaka hiyo ili kuweza kujisajili kwa ajili ya kupatiwa huduma ya maji ili kutimiza lengo la Rais Samia la kumtua Mama ndoo kichwani.
"Leo nimekuja na wajumbe wa Bodi ili kujihakikishia kama kweli zile fedha tunazozihidhinisha kama kweli zinahakisi kilichopo kwenye miradi husika" alisema Mwamunyange
Pia Mwamunyange amesema Bodi imefuatilia na kukagua uchimbaji, ulazaji wa Bomba pamoja na ujengaji wa Pampu za kusukumia maji na wamejiridhisha mradi huo umekamilika kwa asilimia mia hivyo imebaki kazi ya wananchi kuanza kutumia maji ya mradi huo.
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema Mradi wa Maji wa Ruvu Juu hadi Mboga ni Mradi unaenda kuondoa kero ya upatikanaji wa Maji katika maeneo ya Mlandizi, Chalinze na Mji Mdogo wa Mboga, pia Mradi huu umelaza mabomba ya inchi 12 kwa umbali wa Kilomita 59 kutoka mtambo ya Ruvu Juu hadi Chalinze, Mji wa Mboga.
Pia amesema kiasi cha Shilingi Bilioni 18 kimetumika kwenye Miradi wa Maji wa Ruvu Juu mpaka Msoga itakayotatua kero ya Maji kwa wananchi zaidi ya 122,000 wa maeneo hayo hivyo kumalizika kwake itakuwa ndio suluhu la upatikanaji wa maji kwenye mji wa Chalinze, Pingo, Pera, Msoga, Bwilingu, Msata, Kihangaiko, na Ubenazimozi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu toleo(Off take)ya kutoa maji kutoka Mtamboni kwenda kwenye mradi wakati wa ziara ya Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA ya kukagua mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze - Mboga pamoja na Chalinze awamu ya lll.
Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu mtambo wa kusukumia maji wa Ruvu Juu wakati wa ziara ya Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA ya kukagua mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze - Mboga pamoja na Chalinze awamu ya lll.
Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze - Mboga uliogharimu takribani bilioni 18 pamoja uendeshaji wa pampu ya kusukumia maji ya Chamakweza wakati wa ziara ya Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA ya kukagua mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze - Mboga pamoja na Chalinze awamu ya lll.
Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu ka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakimsikiliza Meneja wa DAWASA Chalinze Mhandisi Pascal Fumbuka alipokuwa anatoa taarifa ya wateja ambao wameweza kufungiwa huduma ya maji katika eneo la Chamakweza wakati wa ziara ya Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA ya kukagua mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze - Mboga pamoja na Chalinze awamu ya lll.
Muonekano wa Pampu ya kusukumia maji ya Mboga
Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu Pampu ya kusukumia maji ya Mboga wakati wa ziara ya Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA ya kukagua mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze - Mboga pamoja na Chalinze awamu ya lll.
Ziara ikiendelea
Mwenyekiti wa Bodi Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa ziara ya Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA ya kukagua mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze - Mboga pamoja na Chalinze awamu ya lll.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa mradi wa Mlandizi Chalinze-Mboga uliogharimu sh. Bilioni 18 na kulaza Bomba kubwa za inchi 12 kwa Kilometa 59 mara baada ya kumalizika kwa ziara ya Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA ya kukagua mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze - Mboga pamoja na Chalinze awamu ya lll.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment