Na Abdullatif Yunus - Michuzi Tv Kagera.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amezindua rasmi kampeini ya Upandaji miti aina ya Palm ndani ya Manispaa ya Bukoba, Tukio ambalo limeafanyika katika Viwanja vya Uhuru Platform (mayunga) Machi 18, 2022.
Dkt. Mpango amewaongoza Viongozi wengine wa Dini Serikali na Chama ikiwemo Kamati inayoratibu zoezi hilo la upandaji Miti hiyo aina Palm, katika Uzinduzi Rasmi wa Kampeini ya Kuupamba Mji wa Bukoba ili kufanana na Miji mingine kwa kupanda Miti hiyo yenye kuleta mandhari nzuri ikiwa pia ni utunzaji wa mazingira.
Katika Hotuba yake Makamu wa Rais Amekumbusha Jamii juu ya Umuhimu wa Uhifadhi na Utunzaji wa Mazingira ikiwa ni pamoja na kupanda Miti ya Maua na Matunda.
Kampeni hii inazinduliwa kutokana na juhudi kubwa za Muasisi wa na Mzawa wa Buyekera Bukoba Ndugu Justin Kimodoi anayeishi Marekani, aliyeleta wazo hili na kulieneza kwa Wazalendo wengine waishio nje na ndani ya Nchi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akipanda Palm Tree ikiwa ni ishara ya Uzinduzi wa Kampein ya Upandaji Miti hiyo kwenye Manispaa ya Bukoba yenye lengo la kutunza Mazingira na kupamba Mji.
Viongozi wa Dini wakishiriki kupanda Miti ya Palm, kushoto ni Askofu Abednego Keshomshahara wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi akiwa na Sheikh Yusuph Kakwekwe Sheikh wa Manispaa ya Bukoba, wakiwakilisha Viongozi wengine wa Dini.
Mkuu wa Mkoa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge akishiriki kupanda Mti wake wa Palm katika uzinduzi wa Kampeini ya Upandaji Palm Tree Bukoba.
Mama Costancia Buhiye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa Kagera, akishiriki zoezi la upandaji Palm, akisaidiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Palm Tree Planting Bwana Mkude
Baadhi ya WanaKamati ya Palm Tree Planting na Wazalendo wakishiriki kupanda Mti wao, katikati Mwenye Shati nyeusi ni Naibu Waziri wa Nishati Wakili Stephen Byabato (Mb) ambaye pia ni mjumbe wa kamati. Picha zote na Dulla Uwezo
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment