RIDHIWANI AWAPIGA 'KITANZI' WAVAMIZI WA MAENEO NCHINI MAARUFU ( TEGESHA) | Tarimo Blog



Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze


Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Chalinze ,Ridhiwani Kikwete ametoa agizo kwa wavamizi wa maeneo,nchini wasio fuata sheria na taratibu kwa kueleza kwamba suala hilo ni uvunjifu wa sheria na ni lazima likome mara moja.

Aliyasema hayo wakati akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Diozile kilichopo Chalinze Mkoani Pwani kwenye mkutano wa hadhara ambapo Kijijini hapo pana mgogoro na tatizo kubwa la uvamizi wa maeneo ambapo Wakurya , wamevamia eneo la Kijiji cha Diozile na kufanya shughuli zao za uchomaji wa mkaa na kilimo kinyume na sheria.

"Hakuna nafasi kwa Watu kwenye nchi yetu kuvamia maeneo bila kufuata sheria, Kumekuwa na watu wanaojulikana kama tegesha ambao wamekuwa wakivamia maeneo na kujitegesha ili baadae waonewe huruma na Serikali ili wapewe maeneo hayo. Jambo hili halikubariki." Alisema Ridhiwani.

"Natoa agizo kwa nchi nzima kwamba hakuna nafasi ya kuingia na kuishi sehemu bila kufuata utaratibu."

Alieleza,Watu wanaofanya hivi ni wahalifu kama wahalifu wengine.

Ridhiwani anasema,Utaratibu upo wazi kwa mtu anayetaka kuingia na kuishi sehemu ni lazima afuate sheria kwa kujitambulisha kwa Kijiji husika au Serikali ya eneo analotaka kuishi kwasababu Serikali yetu haikatazi mtu yeyote kuishi popote lakini lazima afuate sheria.

Alisema lazima tumalize migogoro ya ardhi na kudhibiti uvamizi wa maeneo kwasababu nchi haiwezi kuendeshwa kwa watu kuvamia vamia tu maeneo bila kufuata sheria na kuwa na migogoro ya ardhi.

Vilevile,Ridhiwani Kikwete alisema, Machi 07, 2022 huko Chalinze patafanyika kikao cha kugawa Hati zaidi ya 300 na kutoa msimamo wa Serikali kuhusu migogoro mbalimbali ya ardhi ikiwemo migogoro aliyoikuta Kijijini hapo Diozile





 


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2