Na Amiri Kilagalila,Njombe
Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu,Sera,Bunge na Uratibu Dkt.Balozi Pindi Chana ameagiza viongozi wa serikali nchini kuangalia,kukagua na kujiridhisha na ujenzi wa miundombinu ikiwemo ya taasisi za serikali ili kuepuka maafa ya nayoweza kutokea kutokana na athari za mvua.
Dkt.Pindi Chana ametoa agizo hilo wilayani Njombe wakati akikabidhi bati zilizotolewa na benki ya Tanzania Commercial bank tawi la Njombe kwa shule ya sekondari Mfriga.
“Hivi sasa tumeambiwa kutakuwa na mvua zilizozidi wastani,kwa hiyo lazima tuwe makini na kuangalia miundombinu ya taasisi na ofisi za serikali ili wakati wa mvua tusipate changamoto”alisema Balozi Pindi Chana
Aidha ametoa wito kwa wananchi kuahikisha watoto wanakwenda shule kwa kuwa serikali inatumia fedha nyingi kuweka vizuri miundombinu ya elimu na elimu ndio urihi wa mtoto.
Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa kwa niaba ya wananchi wa wilaya hiyo,amemshukuru waziri na bank hiyo kwa kuona umuhimu wa kuifikia shule hiyo ili kuendelea kuboresha kiwango cha taaluma kwa wanafunzi.
Kwa upande wake Martin Wambali meneja wa Tanzania Commercial bank zamani Posta bank ambao ni tawi la Njombe,amesema jukumu lao mojawapo ni kuwa karibu na jamii hivyo wataendelea kushirikiana katika shughuli za maendeleo na jamii.
“Tulipata taarifa kwamba Mfriga wanakosa mazingira mazuri ya kusomea kwa hiyo tukaona tuna fungu letu na huku tuna wateja wetu tukasema lazima tufanye kitu hapa Mfriga”alisema Wambali
Bank hiyo imetoa bati 60 zilizokabidhiwa na waziri Pindi Chana kwa shule hiyo ili kuwezesha kuezeka baadhi ya miundombinu ya shule.
Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu,Sera,Bunge na Uratibu Dkt.Balozi Pindi Chana akikabidhi bati kwa uongozi wa Mfriga katika hafla iliyohudhuriwa na watu mbali mbali wakiwemo wanafunzi na wananchi wa kata hiyo.
Bati zilizokabidhiwa kwa shule ya sekondari Mfriga. Martin Wambali meneja wa Tanzania Commercial bank tawi la Njombe akishukuru kwa wananchi kwa kuendelea kushirikiana na bank hiyo na kuomba kuendelea kuhifadhi fedha zao katika taasisi hiyo ili kujiwekea akiba.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment