Na Muhidin Amri,Mtwara
TATIZO la ukosefu wa maji safi na salama kwa wakazi wa kata ya Mbawala wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara, limepatiwa ufumbuzi baada ya Wakala wa usambazaji maji safi na usafi wa mazingira(Ruwasa)wilayani humo kuanza ujenzi wa mradi mkubwa wa maji.
Mradi huo utakagharimu jumla ya Sh. milioni 804,597.262.90 fedha zilizotolewa na Serikali kupitia mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya ugonjwa wa Uvico-19.
Kaimu meneja wa Ruwasa wilayani Mtwara Mhandisi Aloyece Milyangula alisema,mradi huo utawanufaisha wakazi wa vijiji vya Mwindi,Mbawala,Nang’awanga Nachuma,Misufini,Kilomba Nalunga,Migombani.
Milyangula alisema,ulianza kutekelezwa mwezi Januari na unatarajia kukamilika mwezi Mei mwaka huu ambapo wanufaika wa mradi huo ni wakazi 1,1598.
Alisema,mradi wa maji Mwindi unatekelezwa kwa kutumia mkandarasi na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan,kutoa fedha ambazo zitasaidia wananchi wa vijiji hivyo waondokane na kero kubwa ya maji safi na salama hasa ikizingatia kuwa wananchi wa maeneo hayo hawana chanzo mbadala.
Alisema,mradi utakapokamilika utawanufaisha na kubadilisha maisha ya mtu mmoja mmoja na kuchochea uchumi wa wilaya,mkoa wa Mtwara na Taifa kwa jumla.
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Mwindi Issa Namwewe, ameshukuru kupata mradi huo wa maji kwani kwa muda mrefu kilio kikubwa cha wananchi wake ni ukosefu wa maji safi na salama.
Alisema,wananchi wa Mwindi hawakuwa na chanzo chochote za kupata maji, badala yake walilazimika kwenda kutafuta huduma hiyo kwenye vyanzo vya asili.
Kwa mujibu wake,vyanzo hivyo havikutosheleza mahitaji yao,jambo lililosababisha kero kubwa na wakati mwingine kutumia nguvu na hata kupigana ili kupata maji, ambayo hayakukidhi mahitaji ya familia zao.
Wakati huo huo, Wakala wa maji safi na usafi wa mazingira(Ruwasa)wilaya ya Masasi imepokea jumla ya Sh.milioni 929,135,130.99 za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taif ana mapambano dhidi ya ugonjwa wa Uvico-19.
Fedha hizo ni kwa ajili ya kutekeleza mradi wa maji utakaowanufaisha wakazi 13,442 katika vijiji vinne vya Chidya,Chiwata,Msokosela na Chakama.
Meneja wa Ruwasa wilayani Masasi Juma Yahaya alisema, katika kijiji cha Chidya na Chiwata wananchi watakaonufaika na mradi huo ni 8,622 kijiji cha Chikama wananchi 2,426 na Msokosela ni 2,304.
Kaimu Meneja wa Ruwasa wilaya ya Mtwara Mhandisi Aloyce Milyangula akikagua nyumba ya kuhifadhi mashine ya kusukuma maji kwenye mradi wa maji Mwindi unaotekelezwa na Ruwasa kwa ajili ya kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa vijiji vinavyounda kata ya Mbawala wilayani Mtwara. Kaimu Meneja wa wakala wa maji safi na usafi wa mazingira Ruwasa wilaya ya Mtwara Mhandisi Aloyce Milyangula kulia na Afisa maendeleo ya jamii Clever Paul wakikagua ujenzi wa nyumba ya mtumishi atakayehudumia mradi wa maji wa Mwindi kata ya Mbawala utakaotoa huduma ya maji katika vijiji vya kata hiyo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment