Waziri wa Katiba na Sheria George Simbachawene akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika Taasisi Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo nchini (Law School) leo Machi 10, 2022 Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Tafiti na Machapisho, Law Shool Profesa Zakayo Lukumay akieleza jambo mbele ya Waziri wa Katiba na Sheria George Simbachawene pamoja Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Benhajj Masoud mara baada ya waziri huyobn kumaliza kufanya ziara kwenye taasisi hiyo leo Machi 10, 2022 Dar es Salaam.
Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo nchini (Law School) wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria George Simbachawene baada yanm kumaliza kufanya ziara yake kwenye taasisi hiyo leo Machi 10 2022 Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe.Geofrey Pinda aliyesimama akizungumza na watumishi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheri kwa Vitendo baada ya Waziri wa Katiba na Sheria George Simbachawene kumaliza kufanya ziara kwenye Taasisi ya hiyo leo Machi 10, 2022 Dar es Salaam
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.George Simbachawene akipokelewa na Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo nchini (Law School) Dkt. Benhajj Masoud pamoja na watumishi wa taasisi hiyo kufanya ziara kwenye Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo nchini (Law School) leo tarehe Machi 10, 2022 Dar es Salaam.
WAZIRI wa Katiba na Sheria George Simbachawane amevushauri vyuo vinavyofundisha taaluma ya sheria nchini kuhakikisha wanaweka vitengo vya kutoa msaada wa huduma ya kisheria kwa wananchi wote hasa wale wasiokuwa na uwezo ili kupeleka haki mbele
kama ambavyo shule ya sheria nchini inatoa huduma hiyo.
Waziri Simbachawene ameyasema hayo leo Machi 10 2022, wakati wa ziara yake katika Chuo cha sheria Dar es Salaam.
Amesema kuwa huduma ya msaada wa sheria ipo kwa mujibu wa sheria na kwamba Serikali imeanzisha kitengo hicho " Ofisini kwetu yupo Mkurugenzi anayeshughulika na huduma na anasajili watoa huduma hiyo na wizara hiyo inahakikisha kila mwananchi anapata haki yake
"Nchi yetu bado inahitaji wanasheria ama mawakili ili kusaidia wananchi na Taifa kwa ujumla na ndio maana hivi karibuni serikali imetunga sheria ya msaada wa kisheria ambao unatolewa bure na Taasisi, watu mbali mbali na wizarani ambako kuna mkurugenzi anayehusika na usajili ya huduma hiyo ya msaada wa kisheria ambae pia anawasajili watoa huduma.
"Nakipongeza Chuo hiki kwa kuwa na utaratibu mzuri kwani nimekuta wamefungua kitengo cha msaada wa kisheria na wanatoa huduma hii bure" amesema Simbachawene.
Amesema, amefurahi sana kuona namna wanafunzi wa Chuo hicho wanavyoandaliwa kwenda kutatua changamoto mbali mbali za kisheria kwa wananchi na Taifa kwa ujumla .
Aidha nakipongeza sana Chuo hiki na uongozi mzima kwa kufanikisha ile kazi ambayo serikali ilikusudia ya kuandaa mawakili ili waweze kuwa na uwezo wa kushindana na mawakili wengine dunia na wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
" Saizi dunia inaishi kwenye mitandao katika makubaliano, unapokuwa na wanasheria wazawa ambao wameiva vizuri unakuwa umetengeneza silaha kubwa katika nchi kama vile tunavyoweza kununua silaha za kijeshi katika kulinda nchi", amesema Simbachawene
Aidha Simbachawene amesema, Chuo cha sheria kinaandaa watu kwenda kufanya uwakili na siyo mwanafunzi kufaulu mtihani, kwa hiyo ule uwezo ambao mwanafunzi atakuwa ameupata kuweza kumsaidia mteja wake kwa vitendo ndio utakaomuwezesha kufaulu vizuri.
Amesema, uwakili ni kuongea siyo kuandika hivyo kama wakiingia Chuo wanafunzi mia nane na wakatoka mia mbili sisi tunaamini kuwa Chuo kinafanya kazi nzuri kwa hawa wanasheria wanaotaka hapa wanaenda kusimamia viapo, mikataba kuandaa kuunganisha watu na kusuluhisha mambo mbalimbali.
" Hakuna maneno maneno kwenye taaluma ya sheria kama maeneo mengine, hivyo hatuwezi kuchukua kama mtihani wa shule au vyuo vya kawaida ili wanafunzi watoke tu, hapana ikifanyika hivyo tutakuwa tumearibu maana nzima ya kuwajengea uwezo wanafunzi hawa ili tuweze kuwa na mawakili wazuri katika Kanda na dunia kwa ujumla.
Aidha amesema, Chuo kinahitaji kuwa na vitendea kazi vya kisasa, ili hatimae nao waweze kwenda sambamba na Mhimili wa Mahakama ambao kwa sasa umefika mbali katika masuala ya ICT kwabi sasa unaweza pata huduma za Utabiri kimahakama kutokea mahali popote kwa njia ya mtandao.
Naye, Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Benhajj Masoud amesema wamefarijika na ziara ya Waziri huyo chuoni hapo kwa kuwa imewaongezea hamasa katika masuala mbalimbali na kwamba wataendelea kutimiza majukumu yao hasa katika kuhakikisha wahitimu wanaotoka mahali hapo wanakuwa na weledi wa kutosha.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment