Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
WAZIRI wa Katiba na Sheria George Simbachawene amewasilisha masuala mbalimbali yanayohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa
Akizungumza leo Machi 23,2022 , Waziri Simbachawene ameanza kwa kushukuru na kueleza wamemaliza mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu uliofanyika katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Geneva nchini Uswisi.
"Katika mkutano huo tumepata fursa ya kufanya mapitio maalum ya vigezo mbalimbali kuhusu haki za binadamu,kila mwaka hufanyika tathimini ikiwa pamoja na uchambuzi wa maelekezo mbalimbali yaliyokubaliwa na yale hayajakubaliwa huwekwa kwenye rekodi ili yaendelee kutafakariwa
"Kwa hiyo nimefurahi kupata hii fursa ya kuweza kuzungumza kwenye baraza la Haki za Binadamu na Tanzania tumeeleza hatua kubwa zilizochukuliwa katika mwaka huu mmoja wa uongozi na mabadiliko mengi yaliyofanyika katika masuala ya Haki za Binadamu yanayohusiana na elimu,afya na demokrasia kwa ujumla
"Bila kusahau kwenye mkutano huo tumegusia masuala ya maamuzi na utashi wa Rais wetu Samia Suluhu Hassan ambaye aliruhusu mtoto wa kike aliyepata ujauzito baada ya kujifungua kuendelea na masomo,"amesema Waziri Simbachawene wakati akielezea yaliyojiri kwenye mkutano huo.
Kutoka Kushoto: Balozi Maimuna Tarishi, Mwakilishi wa Kudumu, Geneva, Mh. George Simbachawene Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Hoyce Temu Naibu Mwakilishi wa Kudumu Geneva na Nkasori Sarakikya Mkurugenzi Wizara ya Katiba na Sheria
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment