CCM tawi Mabibo wawanoa watia nia. | Tarimo Blog
CHAMA cha Mapinduzi CCM Tawi la Mabibo mkoani Dar es Salaam kimewapiga msasa wanachama wake na wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kuelekea kwenye uchaguzi wa Mashina ambao unafanyika kesho.
Akizungumza mbele ya wanachama wao wa CCM twi la Mabibo Katibu wa Tawi hilo ambaye anamaliza muda wake Fatuma Ngunji amesema kwaza anamshukuru Mungu Kwani Ameongeza tawi kwa miaka kumi na amejenga umoja na mshikamano.
Amesema katika kuelekea uchaguzi ngazi ya shina wao kama viongozi wamewndesha semina kwa watia nia ili kuwajengea uwezo katika uongozi lakini pia kuwafanya kuwa wamoja, Upendo na mshikamano.
" kama mnavyoona Ndugu zangu waandishi wa habari ndani ya chama Chetu hivi sasa kuna chaguzi mbalimbali zinaendelea na kesho tunaaza ngazi ya shina baadae jumuiya na tunaendelea hivyo hivyo lazima tuwapige msasa"amesema Ngunji
Kwaupande wake mlezi wa Chama hicho Kata ya Mabibo Nafi Habibu amesema kuwa katika Kata ya Mabibo kuna matawi 11 hivyo wao kama wajumbe na sehemu ya viongozi wamekuwa wakitoa semina hiyo ili kuwafanya kuwa viongozi bora na wanaujuwa majukumu yao na kesho chaguzi zinaaza ngazi mashika.
Amesema kuwapa semina watia nia kunawafanya kujua majukumu yao lakini pia kunatoa fursa wanaccm kuwa kitu kimoja na kuwa na Upendo miongoni mwao hivyo lazima washikamane.
Naye Mwenyekiti wa Chama hicho Mohamed mbonde amesema Chama cha Mapinduzi CCM Kina misingi yake hivyo ikiwa panoja na kuwanoa wanachama wake kwa kutoa semina elekezi ili kujua misingi ya uongozi.
Chama hicho hivi sasa kimeaza chaguzi mbalimbali ndani ya chama na wameazia ngazi ya mashina na baadae maeneo mengine na mwisho ngozi ya taifa hivyo ni muda wake wa wanaccm kuchangamkia fursa hiyo. Katika Kiwania nafasi ndani ya chama.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment