FAINI ZINAZOLIPEWA MAHAKAMANI ZIWE CHANZO CHA MFUKO WA MSAADA WA KISHERIA | Tarimo Blog


 Na Mwandishi Wetu

WAZIRI  wa Katiba na Sheria Dkt.Damas Ndumbaro ametaka faini zinazolipwa mahakamani ziwe chanzo cha fedha katika mfuko wa msaada wa kisheria unaotarajiwa kuanzishwa hivi karibuni.
 
Waziri Ndumbaro ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akipokea taarifa ya Kongamano la msaada wa Kisheria lililofanyika mapema mwezi wa nne jijini Dodoma.

Taarifa imewasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Legal Service Facility Bi. Lulu Ng’wanakilala
 
Waziri Ndumbaro alisema “Moja kati ya chanzo cha fedha za mfuko wa msaada wa kisheria ni faini zinazolipwa mahakamani”
 
Pia Waziri Ndumbaro aliwataka watendaji wa LSF na Wizara kujifunza kuhusu uendeshwaji wa Mfuko wa msaada wa Kisheria kutoka kwa nchi nyingine kama Kenya na Zambia ambazo tayari zina mifuko hiyo.
 
Vilevile Waziri Ndumbaro ameshauri kuangaliwa upya kwa mfumo wa haki jinai nchini kwani unaonekana kupitwa na wakati.
 
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Legal Service Facility Bi. Lulu Ng’wanakilala amesema wamekuwa wakishirikiana kwa karibu na Wizara ya Katiba na Sheria tangu kuanzishwa kwa sheria ya Msaada wa Kisheria mwaka 2017 katika kuwawezesha watoaji wa msaada wa kisheria ili waweze kutenda kazi zao.


 
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2