Na Mwandishi Wetu
MAKAMU wa Mwenyekiti wa ChamaCha Mapinduzi (CCM) Taifa, Abdulrahman Kinana, amewataka wafanyabiashara kuorodhesha changamoto zinazowakabili na kumfikishia ofisini kwake ifikapo Mei 5 mwaka huu ili azifanyie kazi.
Alisema hayo Jana usiku kwenye hafla ya Iftar iliyoandaliwa na Kampuni ya Silent Ocean kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam huku ikihudhuriwa na watu mashuhuri.mbalimbali pamoja na wafanya biashara wakubwa nchini.
Kinana alisema hayo jijini Dar es Salaam jana katika maadhimisho ya miaka 18 ya mafanikio ya Kampuni ya kusafirisha mizigo baharini ya Silent Ocean Ltd nchini, iliyohudhuriwa na wafanyabiashara na watu wa kada mbalimbali.
"Pamoja na kuleta changamoto hizo kwangu, zifikisheni pia kwa Waziri husika, lakini mimi nitafuatilia kwa karibu ili kuhakikisha changamoto zinazowakabili zinatatuliwa," alisema Kinana.
Kiongozi huyo alikiri kwamba wafanyabiashara wanakakabiliwa na changamoto nyingi zikiwamo sheria ambazo siyo rafiki kwao, hali ambayo inachangia kuwafanya washindwe kufanya biashara zao kwa ufanisi.
"Nchi hii imeharibiwa imeharibiwa na tuko mbioni katika kutaifanyia kazi na tupeni muda wafanyabiashara mtafurahia matunda ya jasho lenu
Aidha, Kinana aliipongeza Kampuni ya Silent Ocean Ltd na Kimajanjaro Star Cargo kwa kufungua ofisi zake nchini Marekani ili kwamba mtu anayetaka kusafirisha mizigo kutoka huko hadi hapa nchini aweze kupata huduma hiyo.
Awali, Mwenyekiti wa wafanyabiashara Mkoa wa Dar es Salaam Yusuph Yenga aliishikuru serikali kwa kukusanya kodi bila kutumia nguvu, na kwamba wafanyabiashara wanafurahia hatua hiyo.
"Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imetufurahisha kwa hatua hiyo, lakini changamoto bado iko bandarini ambapo utoaji wa mizigo unachukua muda mrefu kuanzia wiki mojan hadi tatu," alisema Yenga.
Mwenyekiti huyo aliiomba serikali iwasaidie kumaliza tatizo hilo, huku Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT), akitaka wamachinga kuondolewa mbele ya mduka ya wafanyabiashara wakubwa Kariakoo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Wazirin Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Innocent Bashungwa iliwataka wafanyabiashara kuipa serikali ushirikiana wakati ikiendelea kuwaboreshea mazingira ya biashara.
"Serikali inatambua changamoto zenu inafanya jitihada za kuweka mazingira rafiki ya kufanya biashara, lakini pia kuweka mazingira rafiki lakini pia kuwe na jukwaa la kukaa na kuzijadili," alisema Bashungwa
Waziri huyo aliongezaa kusema; "Lakini pia mmegusia suala la wamachjinga kwamba wanaziba maduka yenye Kariakoo, ninyi wote ni watoto wa serikali na ipo kwa ajili yenu itawajengea uwezo ili kufikia mafanikio."
Mkurugenzi Mtendaji wa Silent Ocean Ltd na Kilimanjoro Star Cargo, Mohamed Soloka, alisema wamefungua ofisi nchini Marekani ikiwa ni mwendelezo wa kupanua huduma zao.
Ofisi yetu nchini Marekani ipo Washington DC, hivyo kwa wale wanaotala kusafirisha bidhaa zao kutoka kwenda nchi mbalimbali ikiwamo Tanzania, tunaweza kuwahudumia," alisema Soloka.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment