Naibu Spika aipongeza BancABC kwa kuleta suluhisho la kifedha nchini | Tarimo Blog

 
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri wa Tanzania Mussa Azzan Zungu ameipongeza BancABC Tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya Atlas Mara kwa kwa uwekezaji mkubwa ambao benki hiyo imeweza kuwekeza hapa nchini na hivyo kuwa suluhisho la kifedha kwa Watanzania. Zunngu aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akiongea na wateja pamoja na wafanyakazi wa BancABC Tanzania wakati wa futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake.

‘Sekta ya fedha ni nyenzo muhimu sana katika ukuaji wa uchumi wa taifa lolote lile, hivyo unapokuwa na sekta imara ya fedha maana yake ni kwamba uchumi wan chi unakuwa imara. Serikali inatambua jitihada za kukuza uchumi na kupunguza umaskini kuwa na mafanikio bila kushirikisha sekta binafsi hususan taasisi za kifedha’, alisema Zungu huku akisema kuwa BancABC Tanzania imekuwa ni moja ya taasisi ya kifedha ilio imara na yenye kuunga serikali kwenye kufikia suluhisho la kifedha hapa nchini.

Aliongeza kuwa serikali imekuwa ikifanya mageuzi mbali mbali tangu miaka ya 90 kwa nia ya kuiwezesha sekta binafsi hapa nchini na yote ni kwa sababu ya ukuaji wa uchumi wetu. Tangu kuingia kwa mfumo wa soko huria hapa nchini, sekta binafsi imeweza kuchukua nafasi yake katika huduma mbali mbali zikiwemo huduma za za sekta ya kifedha. Sisi kama Bunge na washauri wakuu wa serikali tutaendelea kuhakikisha kuwa uhusiano wa karibu uliopo kati ya serikali na sekta binafsi zikiwemo taasisi za fedha unadumishwa.

Zungu aliongeza, ‘Natambua kuwa BancABC imeendelea kuwa mdau mzuri sana kwenye kuunga mkono juhudi na mikakati ya serikali ya kuongeza tija katika sekta ya huduma za kifedha kwa kupanua huduma zenu ili kuwafikia Watanzania walio wengi Zaidi. Naomba kuchukua fursa hii kuwapongeza kwa juhudi zenu za kuwainua wajasiriamali wadogo kwa kuwapatia mikopo ya biashara pamoja na huduma ya mikopo kwa wafanyakazi wa serikali nchi nzima’.

‘Naomba niwapongeze sana BancABC kwa juhudi zenu kubwa mnazo weka kwenye kupanua huduma zenu ili kuwafikia Watanzania walio wengi na hasa kwenye maeneo ya vijijini. Hii ni hatua kubwa sana na ya kupongezwa kwani kadri mnavyoendelea kuwafikia Watanzania wengi ndipo mnapozidi kuwafungulia milango ya kujiongeza kiuchumi na hivyo kuunga mkono juhudi za serikali za kuongeza kipato kwa wananchi wake,’ Naibu Spika Zungu alisema.

‘Nimepata taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji kuwa BancABC pia imekuwa ikishiriki katika utekelezaji wa masuala ya kijamii ikiwemo kutoa huduma ya bima ya afya kwa Watoto yatima, kushirikiana na Taasisi ya Mheshimiwa Stella Ikupa katika kukuza uelewa wa huduma jumuishi za kifedha kwa watu wenye ulemavu pamoja na kushirikiana na TAMISEMI katika ujenzi wa vyoo na vyumba vya madarasa ya shule mbalimbali nchini. Hii ni ishara tosha kuwa BancABC ni mshirika mzuri katika masuala ya jamii na wanapongeza kwa hilo na kuwaomba kwa Mungu azidi kuwapa nguvu ya kuzidi kufanya Zaidi ya hayo,’ Zungu aliongeza.

Awali, wakati akimkaribishwa Naibu Spika, Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC Tanzania Imani John alisema kuwa BancABC inatoa huduma mbalimbali kwa watu binafsi, wajasiriamali wadogo na wa kati pamoja na wateja wakubwa zikiwemo huduma za kuweka fedha pamoja na mikopo wezeshi kwa wateja wa madaraja yote.

Kwa kipindi ambacho tumekuwa tukitoa huduma, ubunifu wa huduma za BancABC pamoja na mipango yetu madhubuti imepelekea kutambuliwa na wadau mbalimbali katika sekta ya huduma za kifedha na imetupatia tuzo mbalimbali.

Aliongeza kuwa BancABC inazo huduma za kadi za malipo ya kabla, ambazo ni maalum kwa wateja kufanya miamala bila ya kuwa na akaunti kwa njia salama na nafuu kwa malipo ya njia ya mtandao na kwenye mashine za malipo yaani “POS machines” ambazo zimetambuliwa na kupewa tuzo na VISA kwa miaka mitatu mfululizo.

Alisema kuwa kadi hizi zinapatikana katika sarafu sita tofauti ambazo ni Shilingi ya Tanzania, Dola ya Kimerakani, Randi ya Afrika ya Kusini, Pauni ya Uingereza, Yuro ya Ulaya pamoja na Yuan ya China.




Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri wa Tanzania Mussa Azzan Zungu akiwaongoza wateja na wafanyakazi wa benki ya BancABC Tanzania kwenye futari iliyoandaliwa na benki hiyo ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo na shukrani hasa kwa wale ambao wako kwenye mfungo kwa kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.






Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC Tanzania Imani John akiwaongoza wateja na wafanyakazi wa benki hiyo kwenye futari iliyoandaliwa na benki hiyo ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo na shukrani hasa kwa wale ambao wako kwenye mfungo kwa kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC Tanzania Imani John (kulia) akimkabidhi zawadi kwa Naibu Speaker wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Azzan Zungu wakati wa futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jana jijini Dar es Salaam.



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2