Na Mashaka Mhando, Kondoa
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Shaka Hamdu Shaka, Ijumaa ijayo anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye mashindano ya Quran Tajweed yatakayofanyika katika msikiti Mkuu mjini hapa.
Kwa mujibu wa mratibu wa mashindano ya Tajweed, Alhadj Marusu Matata Msii wa Taasisi ya Tabazat Babussalaama ya mjini hapa, alisema yatafanyika April 29 ambayo Kiislamu itakuwa mwezi 27 Ramadhani.
Alisema jumla ya washiriki 50 watashindana kutoka wilaya zote za Mkoa wa Dodoma ambapo Alhamisi wataanza mchujo wa kupata watu 10 watakaoshinda kupata washindi watatu watakaopata zawadi.
Akizungumzia lengo la Tajweed hiyo Alhaj Msii alisema ni kutuitukuza dini ya Kiislamu kupitia kitabu chake Cha Korani ambacho kimeteremshwa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Alisema wageni mbalimbali wamealikwa watapokewa na Mwenyeji wao Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Sheikh Mustapha Rajab Shaaban na viongozi wengine wa wilaya ya Kondoa.
Alhaj Msii alisema mgeni rasmi pamoja na kutoa zawadi kwa washindi watakaoshinda katika mashindano hayo, pia atafungua Kituo Cha Quran kiitwacho Zawiyatul-Ihisan Kilichojengwa katika eneo la Bicha Kondoa.
Alisema kituo hicho kitakacho kuwa ni hosteli ya vijana wa Kiislamu watakaokuwa wakisoma Elimu ya dini ya Kiislamu, pia itakuwa na vyumba vya kulala vya Masheikh wanaofika Kondoa kwa shughuli mbalimbali mjini hapa.
Haya yatakuwa mashindano ya kwanza kufanyika wilayani Kondoa ambayo pia yatahudhuria na wasomaji maarufu wa Tajweed nchini akiwemo Rajal Ayoub na Uncle Idd ambaye ni bingwa wa pili Afrika akitanguliwa na Abdul Baswat wa Misri.
Shaka Hamdu Shaka Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment