Na Mwandishi Wetu
BENKI ya Absa Tanzania imeungana na wadau wengine katika kudhamini mbio za pili za Dar City Marathon zinazotarajiwa kufanyika Jumapili hii.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Masoko na Uhusiano Aron Luhanga alisema mbio hii imeivutia Benki ya Absa kwa namna inavyokuwa haraka.
“Tunaungana na waandaaji katika kukuza utamaduni wa kuzingatia afya njema na pia kulitangaza Jiji la Dar es Salaam duniani,” alisema.
Alisema wafanyakazi wa Absa na wateja watashiriki katika mbio mbalimbali ikiwemo 5km, 10km na 21km.
“Maandalizi yote yamekamilika kwa upande wetu kwa ajili ya mbiohii. Kwa kweli itakuwa fursa nzuri kwa washiriki kuuona Mji wa Dar es Salaam vizuri na kuimarisha afya zao,” alisema.
Kwa mujibu wa Bw. Luhanga, Absa itakuwa na hema katika viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo mbio hiyo itafanyika na kuongeza kuwa washiriki watapata fursa ya kujifunza mengi kuhusu Absa wakitembelea hema.
Alitoa wito kwa washiriki kujisajili mapema ili kuepukana na usumbufu dakika za mwisho.
Kwa mujibu wa waandaaji, bada ya mbio hizo, kutakuwa na tukio la kipekee la kuonesha filamu ya the Royal Tour iliyozinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan nchini Marekani hivi karibuni kama njia ya kutangaza vivutio mbalimbali nchini.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment