GLCA YAANDAA FUTARI KWA WATUMISHI WAKE, YASISITIZA MATUMIZI SAHIHI YA KEMIKALI | Tarimo Blog

Kaimu Mkemia Mkuu wa Serikali, Sabanitho Mtega akihudumiwa futari iliyoandaliwa maalum kwa Watumishi katika Ofisi za Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali zilizopo jijini Dar es Salaam. 
Imam wa Msikiti wa Manyema, Sheikh Hishma Abdallah akitoa nasaha na ujumbe kwa Watumishi na wageni waliohudhuria hafla ya futari hiyo iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GLCA) katika Ofisi zake jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkemia Mkuu wa Serikali, kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GLCA), Sabanitho Mtega akitoa neno la shukrani kwa Watumishi na wageni waliohudhuria hafla hiyo.
 Baadhi ya Watumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GLCA) wakihudumiwa futari iliyoandaliwa katika Ofisi zao zilizopo jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuonyesha upendo, utu wa maisha ya mwanadamu na thamani kwa Waislamu wote wanaotekeleza ibada hiyo ya funga ambayo ni moja ya nguzo ya Kiislamu.

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GLCA) imeandaa futari maalum kwa Watumishi wa Mamlaka hiyo katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo, utu na thamani kwa Waislamu wote wanaotekeleza ibada hiyo ya funga ambayo ni moja ya nguzo ya dini ya Uislamu.

Akizungumza katika hafla ya futari hiyo iliyoandaliwa katika Ofisi za Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkemia Mkuu wa Serikali, Sabanitho Mtega amesema GLCA imeandaa futari hiyo kwa lengo la kuwaunga mkono Waislamu, kushirikiana nao pamoja katika mwezi huu wa matendo mema ya kumcha Mwenyezi Mungu.

“Mfungo wa Ramadhan, unamkumbusha Muislamu na Mtanzania yeyote ambaye sio Muislamu kutenda matendo yaliyo mema, kumcha M/Mungu na kuacha mabaya”, amesema Mtega.

Mtega amesema anaamini mfungo wa Ramadhan unachagiza amani ya nchi, na kuchagiza maendeleo ya nchi kutokana na amani inayotokana na matendo mema ya Wananchi, amesema wanafanya hivyo kuwaweka Waislamu pamoja ili kuimarisha upendo na uhusiano mzuri baina yetu.

“Kila mwaka tunaalika Masheikh waje kujumuika nasi ili kutoa nasaha kwetu ili kukumbusha kila mtu kumcha M/Mungu katika kipindi hiki ambacho wenzetu wanatakiwa kufanya ibada hiyo ya funga”, ameeleza

Akizungumza kuhusu matumizi salama ya kemikali kwa wadau, Mtega amewakumbusha kuhakikisha wanatumia kemikali hizo kwa usalama, pamoja na kutoa wito kwa wadau hao na kuwakumbusha kuwa GCLA inasimamia na kudhibiti matumizi salama ya kemikali. Pia amewasihi kuwasiliana na Taasisi hiyo ili kupata ufumbuzi wanapopata changamoto.

“Tunawasihi wadau wanaotumia kemikali, watumie kemikali kwa kufuata miongozo na maelekezo yote ambayo Taasisi hii inawapa , lakini pia wahakikishe kwamba wanapoingiza kemikali, kwanza wasajiliwe, wawe na vibali vya kuingiza kemikali nchini ili wasipate kero pindi mizigo yao inapoingia nchini.”

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2