KAMPUNI YA BAKHRESA YAFANIKISHA UPANDAJI MITI ZAIDI 2000 HOSPITALI YA MIREMBE DODOMA | Tarimo Blog
Mkurugenzi wa Sheria na Utawala wa Kampuni ya Bakhresa Group, Shani Mligo akiwa miongoni mwa waliopanda miti katika Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili ya Mirembe Dodoma Aprili 30, 2022.Kampuni hiyo imedhamini upandaji miti zaidi ya 2000 kupitia Taasisi ya Habari Development.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dodoma, Ahadi Sinene akipanda mti eneo la Hospitali ya Mirembe. Sinene alimwakilisha aliyetakiwa kuwa mgeni rasmi katika shughuli hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri.
Upandaji miti ukiendelea Mirembe.
Baadhi ya wanafunzi wakishiriki upandaji miti
Askari wa Jeshi la Kujenga Taifa wakipanda miti.
Waandishi wa habari wakishiriki kupanda miti. Kushoto ni Shaban Tolle wa ITV na Joyce Kasiki wa Majira.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Habari Development, Bernard James (aliyevaa shati la bluu katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Sheria na Utawala wa Kampuni ya Bakhresa Group, Shani Mligo, viongozi wengine wa Jiji la Dodoma pamoja na askari wa JKT.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, ujue yaliyojiri katika tukio hilo....
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment