KATIBU MKUU CCM DANIEL CHONGOLO AZINDUA MAFUNZO YA SIKU KUMI KWA MAKADA VIJANA KIBAHA | Tarimo Blog

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Daniel Chongolo akizungumza leo Mei 25, 2022 mkoani Kibaha wakati wakuzindua mafunzo ya siku kumi kwa makada vijana 120 kutoka nchi sita zilizopo Kusini mwa Afrika katika Shule ya Uongozi Mwalimu Nyerere iliyopo hapo.
Mjumbe  wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa  kupitia kundi la vijana Mkoa wa Pwani Khadija Khalid Ismail akizungumza na waandishi wa habari.


makada wa ZANU moja wakiwa ukumbini.


Na Khadija Kalili, Pwani
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Daniel Chongolo leo Mei 25, 2022 amezindua mafunzo ya siku kumi kwa makada vijana 120 kutoka nchi sita zilizopo Kusini mwa Afrika katika Shule ya Uongozi Mwalimu Nyerere iliyopo Kibaha Mkoani Pwani.

Akizungumza wakati akizindua mafunzo ya siku kumi kwa makada vijana kutoka katika vyama vya ANC (Afrika Kusini), Frelimo (Msumbiji), SWAPO (Namibia), ZANUPF (Zimbabwe),MPLA (Angola)na makada wenyeji kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Chongolo amesema kuwa mafunzo haya yatawajengea uwezo makada vijana hivyo wanamatumaini makubwa kuwa baada ya kuhutimu mafunzo haya watapelekuwa chachu kubwa ya Uongozi ndani ya vyama vyao huku akiwataka kuendeleza misingi ya ujamaa na kujitegemea licha ya kuwa hivi sasa dunia imegubikwa na utandawazi wa sayansi na teknolojia huku akiwataka waweze kuleta mabadiliko ndani ya vyama vyao.

"Natoa shukran kwa Chama Cha Kikomunisti Cha China CPC kutokana na udhamini mkubwa wa mafunzo haya kwani wametuwezesha pakubwa." Amesema 

Katibu Chongolo aliongeza kwa kusema kuwa mafunzo haya kwa makada vijana ni muhimu hasa katika kuzungumza na kushauriana mambo ya msingi katika nchi zetu.

"Makada tumieni fursa mliyoipata Shuleni hapa upasavyo hivyo hamna budi kuhakikisha nguvu kazi ya vijana inatumika katika uzalishaji kwenye nyanja ya sayansi na teknolojia" amesema Chongolo.

Amesema kuwa makada hao wataoata fursa ya kutembelea iliyokuwa Kambi ya Wapigania Uhuru Mazimbu Ili waweze kusoma vyema historia ya ukombozi kwa nchi zilizo Kusini mwa Afrika.

Akizungumza kuhusu mafunzo hayo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Taifa kupitia kundi la vijana kupitia Mkoa wa Pwani Khadija Khalid Ismail amesema kwa kupitia mafunzo hayo wataendana na hali ya kidigitali kutokana na kwamba hali ya sasa inaendana na utandawazi ikiwa ni pamoja na kutumia namna ya kupata mbinu za Uongozi.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2