.Maisha duni ya Waandishi kutokana na kutolipwa mishahara kikwazo kikubwa kwa waandishi
Na.Vero Ignatus,Arusha
Baadhi ya sheria zimetajwa kuwa kitanzi kwa vyombo vya habari,Sambamba na hali duni ya maisha kwa waandishi wa habari kutokana na vyombo vingi kushindwa kulipa mishahara kwa wakati , kutolipa kabisa,kwa sababu mbalimbali ikiwamo hali ngumu ya biashara.
Hayo yamesemwa na Salome Kitomari Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika,Tawi la Tanzania, Leo Jijini Arusha katika siku ya uhuru wa vyombo vya habari,kwamba Ushindani usio sawa kwenye matangazo kwa vyombo vya masafa ya ndani na vile vya nje,unaochangia kupunguza mapato kwa vyombo vya ndani ambavyo vimeajiri wengi
Kitomari amesema kuwa kukosekana utaratibu mzuri unaongeza changamoto ya ajira pamoja na kulipa wanahabari,pia ipo changamoto ya kodi ambayo ni kilio cha wamiliki wa vyombo hivyo vya habari
Aidha ameishukuru serikali kwa kuona changamoto za sheria zinazosimamia taaluma ya habari na kuanza kuchukua hatua mbalimbali,ikiwamo mabadiliko ya kanuni ambayo yalikwaza kazi ya habari,ameipongeza jitihada zilizopo sasa za kuwashirikisha wadau wote kupitia sheria za habari, ili kuondoa vifungu vinavyokwaza pande zote na kuomba wadau wote tushirikishwa kikamilifu.
Aidha ameainisha Malengo ya kuwepo kwa MISA ni kuhakikisha uhuru wa vyombo vya habari na upatikanaji wa taarifa unakuwepo,ukuaji wa vyombo vya habari imara vinavyowajibika na mazingira mazuri ya uandishi wa habari katika nchi wanachama kwa maendeleo na ustawi wa nchi zetu.
Kitomari amesema mengi la MISA-TAN ni kuhakikisha umma unapata taarifa,na ndiyo maana kila Septamba katika right to know Day MISA Tanzania hutoa kufuli kwa taasisi za umma ambao zilifungia taarifa na funguo kwa zilizofungulia taarifa.
"Hii hufanyika kwa utafiti kwa kupeleka maombi ya taarifa kama mwananchi wa kawaida kwenye ofisi husika,kuwaandikia barua pepe zilizowekwa hadharani kwenye tovuti ,kuwapigia simu kwa namba walizoweka kwenye tovuti,lengo ni kuona namna gani mwananchi wa kawaida kabisa anapata taarifa za maendeleo kwa urahisi na kuongeza uwajibikaji kwenye kutoa taarifa kwa taasisi za umma"alisema Kitomari.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment