Naibu Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Juma Mkomi akitoa maelekezo juu ya ukarabati wa juu ya ukarabati wa gati na gereza la Mjerumani wakati wa ziara yake ya ukaguzi miradi hiyo inayotekelezwa na Makumbusho ya Taifa la Tanzania.
Mmoja wa wazee wa Mji Mkongwe wa Mikindani, Bw Selemani Almas akitoa maelezo juu ya jengo alolokuwa akifikia Mwl Julius K. Nyerere wakati wa harakati za kudai uhuru kwa Naibu Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Bw Juma Mkomi katikati kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Bw Dastan Kyobya.
Naibu Katibu Mkuu, Maliasili na Utalii, Juma Mkomi (wa pili kushoto mwenye kofia) akitembea katika mitaa ya Mji Mkongwe wa Mikindani alipotembealiea mji huo kwa jili ya kukagua miradi ya ukarabati wa maghofu. Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Dastan Kyobya na Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa, Dkt. Noel Lwoga (mwenye suti)
************************
Na Joyce Mkinga, Mikindani,
Wadau wa Maliasili nchini wametakiwa kuboresha miundombinu, huduma na ukarimu kama sehemu ya maandalizi ya kupokea wageni wengi wanaota rajiwa kuja nchini kwa matokeo chanya ya Royal Tour.
Naibu Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Bw. Juma Mkomi amesema hayo katika ziara yake ya kutembelea mji wa kihistoria wa Mikindani, Mtwara na kukagua miradi ya UVIKO 19 inayoyekelezwa na Makumbusho ya Taifa.
Bw. Mkomi amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa sana ya kuutangaza utalii wa Tanzania kupitia Royal Tour hivyo, wadau wanatakiwa kujiandaa kupokea watalii watakaokuwa kutembelea Tanzania.
Amesema Mji wa kihistoria wa Mikindani ni eneo muhimu katika utalii wa historial, malikale na utamaduni hivyo, ni eneo ambalo linatarajiwa kupata wageni wa kutosha.
Amesema Mhe. Rais ameonesha njia ya kuutangaza utalii nchini hivyo, wadau wa utalii wanatakiwa kuendelea kutangaza na kuboresha miundombinu, na ukarimu katika maeneo yao ili watalii watakapokuja wafurahishwe na huduma zinazotolewa ili wakaendelee kuutangaza utalii wa Tanzania katika zingine.
“Utalii uliopo hapa Mikindani ni tofauti kabisa na utalii unaopatikana maeneo mengine na umekuwa ukibadilika kwa kasi kutokana na juhudi za wadau katika kuhifadhi mji huu” amesema Bw. Mkomi.
Naibu Katibu aliyetembelea mikindani kwa lengo la kukagua utakelezaji wa mradi wa ukarabati wa majengo ya kihistoria ikiwemo jengo alilokuwa akifikia Mwl Julius Kambarage Nyerere wakati wa harakati za kudai uhuru, gereza la wajerumani, Soko la watumwa na gati katika bahari iliyopo mbele ya gereza.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Bw. Dastan Kyobya amesema kuwa amefurahishwa na kazi inayoendelea katika Mji wa Kihistoria wa Mikindani ya kukarabati majengo ya kale kwa lengo la kuhifadhi urithi wa asili na utamaduni wa mji huo.
Amesema kuna haja ya kutoa elimu kwa wananchi wa Mikindani ili waendelee kuhifadhi majengo hayo kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
“Hili ni eneo muhimu tunalotakiwa kulihifadhi kwa manufaa ya kizazi hiki cha sasa na kijacho kwa sababu kukiwa na mipango mizuri wananchi watafaidika na uhifadhi kwa wakati wa sasa na ujao pia,” amesema Bw Kyobya.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment