KATIKA kuonyesha mwanamke anatimiza ndoto na kuwa kinara katika jamii bila kuwa na changamoto mbalimbali zitakazo mkatisha tamaa katika kufikia malengo yake, Taasisi isiyo ya kiserikali ya Victoria Foundation imetoa msaada wa taulo za kike kwa wasichana 3680 Mkoa Mtwara na 1878 Kwa Mkoa wa Lindi ambako Imekabidhiwa Wilaya ya Ruangwa. pamoja na baadhi ya vifaa vya shule vikiwemo viatu kwa wale ambao hawakuwa navyo.
Msaada huo umetolewa na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Vicky Kamata ambaye licha ya kutoa msaada kwa wasichana hao walipewa elimu ya kujilinda na kujitambua na kusema kuwa "Taasisi hiyo imeamua kujitokeza mbele na kuja kumuinua msichana na kumpa nguvu katika kile kinacho onekana ni tatizo kwa baadhi ya wasichana ambao wanatamani kufikia ndoto zao lakini wanakwamishwa na vitu vidogo vidogo ikiwemo kukosa taulo za kike, Hivyo basi taasisi hiyo imeamua kutoa kidogo walicho nacho ili kuonyesha kuwa Tanzania na Dunia kwa ujumla kuwa kuna haja ya kusaidia wasichana katika changamoto wanazopitia ili kumpa mwanamke kujiamini"
Misaada hiyo imepokelewa na Meya wa manispaa ya Mtwara Bi Shadya Ndile ambaye ameishukuru Taasisi ya Victoria kwa msaada huo ambao ameahidi kiwafikia walengwa na kuwaomba wadau wengine kujitokeza na kuwasadia watoto wa kike na wenye uhitaji.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment