KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Francis Michael amewasisitiza watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa wanyamapori Tanzania (TAWA) Kanda ya Kaskazini kuendelea kuongeza ufanisi na tija ktk ulinzi wa rasilimali za wanyamapori na biashara ya utalii
Dkt. Francis amesema hayo alipotembelea Makao Makuu ya Ofisi ya Kanda-Kaskazini (NJIRO) jijini Arusha kwa lengo la kukutana na wafanyakazi.
Aidha Katibu Mkuu pamoja nakupokea taarifa fupi iliwaaasa watumishi kujiepusha kabisa na vitendo vya rushwa kwani imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa Taifa kupoteza mapato.
Awali, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mhifadhi - Mbanjoko Peter, akitoa taarifa fupi ya kazi zinazofanyika, changamoto, mikakati na utekelezaji wa miradi ya uviko, alimweleza Katibu Mkuu kuwa Tawa Kanda ya Kaskazini imekuwa ikipambana na changamoto mbalimbali ikiwemo muingiliano wa wamatumizi ya ardhi ktk maeneo ya mapori Tengefu (GCA) mbao unatishia ustawi wa Uhifadhi.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment