Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Nelson Swai akitoa mada kuhusu masuala ya fedha zinazovuka mipaka Kidigitali na ujumuishi wa kifedha barani Afrika jijini Dar es Salaam hivi karibuni kwa baadhi ya wamiliki chipukizi wa mifumo ya Tehama wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya ufunguaji wa akaunti za benki za mtandaoni katika nchi mbalimbali na kufanya miamala kwa sarafu yoyote kwa makato madogo kwa kutumia proramu ya Grey ipatikanayo playstore na Appstore. Bwana Nelson alisema DCB imejizatiti katika matumizi ya teknolojia za kisasa katika utoaji wa huduma za kibenki.
Mkurugenzi wa Uendeshaji na Tehama wa Benki ya Biashara ya DCB, Nelson Swai ( kushoto) akizungumza jijini Dar es Salaam mara baada ya kutoa mada kuhusu Masuala ya fedha zinazovuka mipaka kidigitali na ujumuishi wa kifedha barani Afrika wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya ufunguaji wa akaunti za benki za mtandaoni katika nchi mbalimbali na kufanya miamala kwa sarafu yoyote kwa makato madogo kwa kutumia proramu ya Grey ipatikanayo playstore na Appstore. Kushoto kwake ni Meneja Miradi wa Ecobba, Bi. Idabente Winfried, Mkurugenzi wa laina Finance, Tonny Missokia na Mwanzilishi wa Jukwaa Afrika, Baraka Mafole. Bwana Nelson alisema DCB imejizatiti katika matumizi ya teknolojia za kisasa katika utoaji wa huduma za kibenki.
Mmoja wa wamiliki wa mifumo ya Tehama chipukizi (startup) akiuliza swali kwa Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Benki ya DCB, Nelson Swai (hayupo pichani) mara baada ya kutoa mada kuhusu Masuala ya fedha zinazovuka mipaka Kidigitali na ujumuishi wa kifedha barani Afrika katika hafla ya uzinduzi wa huduma za kufungua akaunti za benki za mtandaoni kwenye nchi mbalimbali na kufanya miamala kwa sarafu yoyote kwa makato madogo kwa kutumia proramu ya Grey ipatikanayo playstore na Appstore. Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Bwana Nelson alisema DCB imejizatiti katika matumizi ya teknolojia za kisasa katika utoaji wa huduma za kibenki.
Mkurugenzi wa Uendeshaji na Tehama wa Benki ya Biashara ya DCB, Nelson Swai ( katikati) akizungumza na baadhi ya wamiliki chipukizi wa mifumo ya Tehama wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ufunguaji wa akaunti za benki za mtandaoni katika nchi mbalimbaki na kufanya miamala kwa sarafu yoyote kwa makato madogo kwa kutumia proramu ya Grey ipatikanayo playstore na Appstore. Bwana Nelson alisema DCB imejizatiti katika matumizi ya teknolojia za kisasa katika utoaji wa huduma za kibenki.
Ofisa Huduma kwa Wateja wa Benki ya DCB, Ulumbi Dyamo (kushoto), akisalimiana na Mwanadiplomasia mkongwe na mfanyabiashara maafuru nchini, Balozi Ami Mpungwe aliyefika katika banda la DCB wakati wa kongamano kuhusu ubunifu, teknolojia na ujasiriamali kwa maendeleo ya Taifa liitwalo 'potensial unleashed' lililofanyika katika Hoteli ya Rotana jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Baadhi washiriki wa Kongamano kuhusu ubunifu, teknolojia na ujasiriamali kwa maendeleo ya Taifa wakimsikiliza Ofisa Huduma kwa Wateja wa DCB, Ulumbi Dyamo (kushoto) akiwaelezea manufaa mbalimbali ya kutumia huduma bora za kibenki za DCB, hususan huduma ya DCB Pesa na huduma nyingine kwa njia za Kidigitali katika kongamano lililopewa jina la pontential unleashed jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment