Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akipokea mashine moja kati ya 22 za kutolea dawa kwa kutumia sindano kwa wagonjwa mahututi (syringe pump) kutoka kwa Daktari bingwa wa moyo Michael Schupp zilizotolewa na Hospitali ya Glenfield Leicester iliyopo nchini Uingereza kwa ajili ya Taasisi hiyo zenye thamani ya shilingi milioni 90.2 leo wakati wa kufunga mafunzo ya siku tatu ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi.
Mkurugenzi wa Idara ya Upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela Muhozya akiwa na Daktari bingwa wa moyo kutoka Shirika la Cardio Start la nchini Marekani Michael Schupp na Daktari kutoka Taasisi ya Taifa ya Tafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dkt. Kunda John wakijadili kuhusu mashine 22 za kutolea dawa kwa kutumia sindano kwa wagonjwa mahututi (syringe pump) zenye thamani ya shilling milioni 90.2 zilizotolewa na Hospitali ya Glenfield Leicester iliyopo nchini Uingereza kwa ajili ya Taasisi hiyo wakati wa kufunga mafunzo ya siku tatu ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi.
Picha na Khamis Mussa
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi cheti cha ushiriki wa mafunzo ya kuwahudumia wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum na mahututi mshiriki wa mafunzo hayo kutoka JKCI AfIsa Muuguzi Aimana Nkya wakati wa kufunga mafunzo hayo leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi cheti cha ushiriki wa mafunzo ya kuwahudumia wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum na mahututi mshiriki wa mafunzo hayo kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Dkt. Zainab Hassan wakati wa kufunga mafunzo hayo leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Daktari bingwa wa moyo kutoka Shirika la Cardio Start International la nchini Marekani Michael Schupp pamoja na daktari bingwa wa usingizi na wagonjwa mahututi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Faraji Lydenge wakikagua mashine 22 za kutolea dawa kwa kutumia sindano kwa wagonjwa mahututi (syringe pump) zenye thamani ya shilingi milioni 90.2 zilizotolewa na Hospitali ya Glenfield Leicester iliyopo nchini Uingereza kwa ajili ya Taasisi hiyo leo wakati wa kufunga mafunzo ya siku tatu ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi Mkuu wa Kitengo cha usingizi na wagonjwa mahututi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Faraji Lydenge mashine moja kati ya 22 za kutolea dawa kwa kutumia sindano kwa wagonjwa mahututi (syringe pump) zenye thamani ya shilingi milioni 90.2 zilizotolewa na Hospitali ya Glenfield Leicester iliyopo nchini Uingereza kwa ajili ya Taasisi hiyo leo wakati wa kufunga mafunzo ya siku tatu ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment