· * Yaendelea kupata hati safi kutoka ofisi ya mkaguzi wa Vyama vya Ushirika, kuendelea na mpango wa kusaidia jamii
CHAMA Cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO,) ‘ TANESCO Saccos’ kimefanya mkutano mkuu wa mwaka 2022 huku wakijivunia mafanikio makubwa ikiwemo kupata hati safi kutoka kwa mkaguzi wa Vyama vya Ushirika pamoja na kukua kwa akiba kutoka shilingi 39,879,206,954.00 Mwezi Disemba 2020 hadi kufikia 41,959,533,244.00 kwa mwaka 2021 na kufanya ongezeko la asilimia 5.2.
Akizungumza katika mkutano mkuu wa mwaka 2022 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa TANESCO Saccos Somoe Nguhwe amesema katika mkutano huo mkuu uongozi umekutana na wawakilishi wa wanachama 6000 na kupitia taarifa ya fedha ya mwaka 2021 pamoja na mipango, mikakati na utekelezaji wa mikakati ya kuboresha zaidi ushirika huo.
‘’Tutapitia taarifa ya fedha ya mwaka uliopita pamoja na kujadili utekelezaji wa mipango kwa mwaka wa fedha unakuja, tumepiga hatua kwa mafanikio ikiwemo kupata hati safi kutoka kwa mkaguzi wa Vyama vya Ushirika,pamoja na kukua kwa akiba hadi kufikia asilimia 5.2.’’ Amesema.
Aidha amesema, jumla ya mikopo iliyotolewa kwa mwaka 2021 ilifikia shilingi Bilioni 48,908,423,591.00 ikilinganishwa na shilingi 45,870,262,030.00 iliyotolewa mwaka 2020 sawa na ongezeko la asilimia 7.
Akieleza namna ushirika huo unavyoleta manufaa kwa jamii Bi. Salome amesema wanachama wamekuwa wakinufaika na mikopo inayowasaidia katika miradi mbalimbali ya kijamii na wamekuwa na msingi wa kujali jamii na kwa mwaka huu wameandaa shuka 9000 watakazokabidhi kwa hospitali saba ikiwemo Taasisi ya Saratani Ocean Road.
Akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Maharage Chande, Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa TANESCO Francis Sangunaa amesema vyama vya Ushirika ni msingi katika kujenga maendeleo binafsi na taasisi na kuwahimiza wafanyakazi waliopo na wafanyakazi wapya kujiunga na ushirika huo kwa maendeleo yao binafsi na Taifa kwa ujumla.
‘’ Kati ya wafanyakazi 7000, wafanyakazi 6000 ni wanachama wa TANESCO Saccoss, niwahimize wafanyakazi wengine wajiunge na kuweza kukopa kwa manufaa ya kuinua vipato vyao na Taifa kwa ujumla.’’ Amesema.
Sangunaa amewapongeza wanachama hao kwa kuendelea kuumarisha ushirika huo na kuutaka uongozi kuendelea juhudi za ofisi ya ushirika huo itakayosaidia kuimarisha huduma za chama, kuongeza mapato na kupunguza gharama za matumizi na kueleza kuwa makubaliano ya ushirika huo na TANESCO Ltd utasaidia katika ukusaji wa mapato ya wanachama kwa wakati zaidi kutoa kwa mwajiri.
Pia amewapongeza kwa kutumia mifumo ya TEHAMA katika suala la mikopo kwa wanachama na kuwataka wanachama hao kutumia teknolojia hizo kupitia huduma zinazotolewa ikiwemo huduma za Chama kiganjani.
Mmoja ya wanachama wa Ushirika huo Bi. Monica Massawe amesema kupitia TANESCO Saccos alifanikiwa kujiendeleza kimasomo pamoja na kusomesha watoto na amekuwa mnufaika kwa kuendesha miradi mbalimbali ikiwemo ufugaji na kutoa wito kwa wanachama kujiunga na Saccos hiyo ili waweze kukopa na kujijenga kiuchumi.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa TANESCO Francis Sangunaa amesema vyama vya Ushirika ni msingi katika kujenga maendeleo binafsi na taasisi na kuwahimiza wafanyakazi waliopo na wafanyakazi wapya kujiunga na ushirika huo kwa maendeleo yao binafsi na Taifa kwa ujumla.
Mwenyekiti wa kikao Bi. Monica Massawe akiongoza kikao hicho.
Baadhi ya wanachama wakipokea tuzo kwa utumiaji bora wa huduma, uwekaji akiba na mikopo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment