Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
OFISA Mtendaji Mkuu wa Watumishi Housing Investments Dkt.Fred Msemwa amewashauri wawekezaji nchini kujitokeza ili kuchangia fursa ya Mfuko mpya wa “Faida Fund “ambao umeanzishwa na shirika hilo ili kusaidia wawekezaji kupata faida huku akiwakikishia salama wa fedha zao.
Ushauri huo umetolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Watumishi Housin Dkt. Fred Msemwa wakati wa mkutano wa wadau wa uwekezaji wa mfuko mpya wa faida Fund unaosimamiwa na Watumishi Housing pamoja na Benki ya CRDB Plc ikiwa ni kuwezesha Watanzania kuwekeza kwa kununua hati fungeni kwa bei nafuu kuanzia 5000, na kuendelea.
"Mkutano huu wa leo umewakutanaisha wadau wa sekta za fedha ikiwemo Benki takribani 50 zilizopo hapa nchini Tanzania, Mawakala wa soko la hisa Dar es salaam ( DSE). Aidha Watumishi Housing Investments inauza vipande vya mfuko wa Faida Fund kwa kuwa bado kuna fursa kubwa kwenye Masoko ya fedha.
"Hivyo mtu au kampuni itakayowekeza atanufaika na mfuko huo.Mfuko huu utafunguliwa Novemba 1,2022 na tunawahakikishia wadau usalama wa mfuko huu ni mkubwa kwani unasimamiwa na kuidhinishwa na mamlaka ya serikali ya mitaji na Masoko CMSA, "amesema Msemwa.
Pia kutakua na mfumo maalum wa kufanya malipo kwa mitandao ya simu, au mwekezaji anaweza kwenda moja kwa moja kwenye ofisi za Benki au ofisi za Watumishi Housing Investments.
Amefafanua usimamizi wa kisheria wa Mfuko wa “Faida Fund” utasimamiwa na Serikali na wawekezaji wanaweza kubaki kwenye uwekezaji wake milele au wanaweza kuacha pale watakapoamua mfuko kuufunga.
Kwa upande wake Mkuu wa Masoko na Mitaji kutoka Benki ya CRDB PLC, Masumai Ahmed Hashimu amewahakikishia wawekezaji kuwa fedha zao watakazoziwekeza kwenye Faida Fund zitakua salama na kwamba ni wakati sasa wa Watanzania kutumia mfuko huo kupata utajiri.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Watumishi Housing Investments Dkt. Fred Msemwa akizungumza katika mkutano wa wadau wa uwekezaji wa Mfuko wa Faida Fund katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere leo Jijini Dar es Salaam.
Meza kuu ikiwasiliza wadau wa uwekezaji wa Mfuko wa Faida Fund.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Watumishi Housing Investments Dkt. Fred Msemwa akijibu maswali aliyoulizwa na wadau wa uwekezaji wa Mfuko wa Faida Fund.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Watumishi Housing Investments Dkt. Fred Msemwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amewaomba wawekezaji kujitokeza ili kuwekeza kwenye Mfuko mpya wa Faida Fund ambao umeanzishwa na shirika hilo ili kusaidia wawekezaji kupata faida leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Watumishi wa (WHI)
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAAKA WA MICHUZI TV)
Wadau wa uwekezaji wa Mfuko wa Faida Fund wakimsikizaAfisa Mtendaji Mkuu wa Watumishi Housing Investments Dkt. Fred Msemwa (hayupo pichani) wakati akijibu maswali.(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAAKA WA MICHUZI TV)
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment