ZAIDI YA WANANCHI 7.200 WAFIKIWA NA ELIMU YA SHERIA NA NAMNA BORA YA KUTATUA MIGOGORO KWA NJIA YA USULUHISH JAJI DK MLYAMBINA AWATAKA WADAU KUONGEZA KASI YA KUSIKILIZII MASHAURI | Tarimo Blog

Na Muhidin Amri, Songea

ZAIDI ya wakazi 7,200 wamefikiwa na elimu ya sheria na namna ya kumaliza migogoro kwa njia ya usuluhishi katika muda wa wiki moja ya maadhimisho ya sheria yaliyoanza tarehe 22  hadi tarehe 29 Januari mwaka huu wilyani Songea.

Hayo yamesemwa na  Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Songea Dkt Yose Mlyambina, wakati akifunga maadhimisho ya wiki ya sheria  ambayo kanda ya Songea yamefanyika katika viwanja vya Mahakama kuu wilayani Songea.

Jaji Mlyambina,amewataka wadau utoaji haki kuongeza juhudi katika kutatua changamoto mbalimbali ikiwamo mashauri na migogoro ya ardhi ili jamii iweze kupata haki kwa wakati.
Alisema,migogoro  na mashauri yakimalizwa ipasavyo itawezesha kuharakisha maendeleo ya mtu mmoja mmoja na kuharakisha uchumi wa nchi kwa kuwa jamii itapata nafasi kubwa ya kujikita kwenye shughuli za uzalishaji mali.

Kwa mujibu wa Jaji Mlyambina,usuluhishi  ni  moja ya njia sahihi na nzuri za kutatua migogoro mbalimbali katika jamii na kuomba wadau wa mahakama kuongeza nguvu na kuharakisha utatuzi wa mashauri yanayofikishwa katika maeneo yao kwa njia hiyo.

Aidha amewataka wadau hao kujikita zaidi katika mfumo wa utoaji haki  kuendelea kutoa elimu kwa umma na kuhakikisha huduma mbadala ya usuluhishi inapatikana na kufikiwa kwa urahisi na kuimarisha utatuzi ili kufikia malengo.

Katika hatua nyingine Jaji Mlyambina amewaasa mawakili wa kujitegemea kujielekeza katika kutoa elimu na ushauri sahihi kwa wateja wao kuhusu namna bora ya kutatua migogoro ikiwa ni pamoja na kutumia njia mbadala ya usuluhisi badala ya kuendelea na kesi mahakamani ambako watalipwa gharama kubwa zaidi za kutetea wateja wao.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Thomas Laban amempongeza Jaji mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Songea Dkt Yose Mlyambina kwa kwa kusimamia vizuri suala ya utoaji haki kwa wananchi wanaofika mahakamani kwa ajili ya kutafuta na kudai haki zao za msingi.

Laban alisema,tangu alipofika mkoani Ruvuma kama Mkuu wa mkoa na mwenyekiti wa kamati ya maadili kwa Mahakimu hajapokea malalamiko yoyote kutoka kwa wananchi wakilalamikia kunyimwa haki na mahakimu au wadau wengine wa sheria.

Alisema,utatuzi wa migogoro iliyopo katika jamii ni haki ya msimgi ya kila mtu ambapo amewataka mahakimu na watumishi wengine wanaofanya kazi katika vyombo vya kusimamia na kutoa haki kuongeza nguvu na kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi na haki badala ya kutatua migogoro kwa upendeleo.

Mkuu wa mkoa,ameliomba Jeshi la Polisi kama wadau wakubwa wa Mahakama nchini,kuanza kutatua migogoro kwa njia ya kusuluhisha migogoro inayofikishwa kwenye vituo vya polisi na kutosita kutoa ushauri  kwa wananchi kumaliza tofauti (migogoro) yao kwa njia ya amani badala ya kufikishana mahakamani.

Aidha,amewaagiza wenyeviti wa mabaraza ya ardhi na nyumba kuongeza kasi ya kusikiliza mashauri ili wananchi wapate muda wa kuendelea kufanya kazi nyingine za uzalishaji mali na siyo kutumia muda wao mwingi kwenda kusikiliza mashauri.

Katibu wa Baraza kuu  la Waislamu(Bakwata)mkoani Ruvuma  Rajabu Songambele,amewataka watumishi wa mahakama k kutunza siri za serikali  na kutenda haki kwa wananchi wengine ili kuepusha nchini kuingia kwenye migogoro inaweza kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.

Alisema,watumishi na wasimamizi wa sheria nchini,ni vyema wakatenda haki kwa wananchi wanaofika katika maeneo yao ya kazi  kudai na kutafuta haki zao, badala ya kupendelea upande usio kuwa na nguvu  ya kifedha au madaraka.

Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS) mkoa wa Ruvuma Edson Mbogoro,ameipongeza Mahakama nchini kwa kufanya mabadiliko makubwa ya kiutendaji  ambayo yanakwenda kuisaidia jamii kupata haki  kwa wakati.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2