KAMPUNI YA GF TRUCKS, STAMICO WAINGIA MAKUBALIA KUWAINUA WACHIMBAJI WADOGO NCHINI | Tarimo Blog
Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
KAMPUNI ya Gf Truck & Equipments Lt kupitia kampuni yake ya ukodishaji wa mitambo ya RENTO MACHINE wamesaini makubaliano na Shirika la Madini nchini (STAMICO)kwa ajili ya kuwasaidia na kuwainua wachimbaji wadogo wa madini ili kuongeza pato lao na pato la taifa.
Pia imeelezwa kwa kufanya hivyo kutaongeza morali kwa wachimbaji wadogo ambao hawana uwezo wa kununu mashine hizo za kuchimbia huku ikielezwa Gf Trucks & Equipment’s ambao ni wauzaji wa mitambo ya kuchimbia ya XCMG na AJAX wanautaratibu wa kuwakopesha wakandarasi wadogo wa miradi mbali mbali ya serikali kwa dhamana na mtambo husika kupitia beki rafiki ambayo Mkandarasi mwenye mradi anaweza akakopesha vitendea kazi na akalipa kwa awamu.
Akizungumza leo Aprili 5,2023 wakati wa kusaini makubaliano hayo Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya GF Salman Karmali amesema wamegundua wachimbaji wengi wadogo hawana mitaji ya kununua mitambo hiyo na kutokana na hilo wameamua kuingia makubaliano na STAMICO S ya kuwakodisha mitambo maalumu ya kuchimbia kwa gharama nafuu .
"STAMICO kama walezi wa wachimbaji madini nchini ni rahisi kumtambua mhusika mwenye mahitaji na kwa kufanya hivyo tutapunguza ajali nyingi zinazotokea migodini kwa wachimbaji kutumia njia za asili , hivyo sasa tumekuja kama mkombozi wao kupitia XCM na AJAX tutakua tumetatua changamoto zao kwa kiwango kikubwa."
Kwa upande wake Naumu Mwakasita akizungumza kwa niaba ya wachimbaji wadogo amesema wao wameichukulia hiyo kama fursa inayokuja kuwakomboa na hali ya kutumia vifaa duni katika uchimbaji, hivyo yeye atakuwa wa kwanza kuchangamkia fursa hiyo na kuachana na uchimbaji kwa kutumia njia za asili ambazo ni hatari
Wakati huo huo Waziri wa Madini Dotto Biteko amewataka wachimbaji kuchangamukia fursa ya kutumia mitambo hiyo kwani inakwenda kuongeza thamani ya madini na kuweza kupata madini yenye ubora. “Ninazo taarifa wachimbaji wengine wamekuwa wakichanganya na vitu vingine ili kuongeza uzito, mfano unachimba gympsum umeshaipata lakini unaamua kuchukua mchanga usiokuwa na thamani yoyote ili kuongeza uzito wa mzigo wako,” amesema.
Amesema kwa kufanya hivyo wamekuwa wakiwatia hasara wenye viwanda jambo ambalo linaweza kuwafanya kufilisika, kufunga viwanda na kuwafanya wao kama wachimbaji wakose soko.“Kuweni waaminifu, kama hauiogopi Serikali basi muogope Mungu, hakuna mtu mwenye akili yake timamu anayeweza kuagiza malighafi kutoka nje kama hiyo malighafi anapata hapa nchini kwa bei nafuu na safi."
Waziri Biteko amesema kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa wachimbaji wakieleza kupunjwa fedha na wenye viwanda kwa kukatwa baadhi ya tani na wanunuzi kwa kuhofia kuwa zitakuwa na takataka.“Kama mtu amepeleka gari lake la tani 30, tani 3 zinakatwa na kuhesabiwa kama ni uchafu, wanampunja mchimbaji kuanzia kwenye uzito na wakati mwingine katika kutumia bei elekezi.
Aidha amesema ni vyema kuwapo kwa ushirikiano thabiti kwani sekta ya madini ya viwandani ni moja kati ya zinazokuwa kwa kasi, ndani ya miaka miwili ya Rais Samia Suluhu Hassan, mapato yake yamefikia Sh.trilioni 1.19 kutoka Sh.milioni 456.
Waziri wa Madin, Dotto Biteko akimpongeza na kumkabidhi chet Mkurugenzi wa Masoko na mawasiliano wa kampun ya GF, Salman Karmali baada ya kusaini mkataba na STAMICO wa kuwakodisha mitambo ya kuchimbia madini wachimbaji wadogo nchini wakati wa mkutano wa wachimbaji wadogo wa madini jijini Dar es salaam
Mkurugenzi wa Masoko na mawasiliano wa kampun ya GF, Salman Karmali akibadilishana nyaraka na Mkurugezi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse baada ya kusaini mkataba wa kuwakodisha mitambo ya kuchimbia madini wachimbaji wadogo nchini wakati wa mkutano wa wachimbaji wadogo wa madini jijini Dar es salaam jana.Kushoto ni Afisa Mauzo wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd , Peter William
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment