SERIKALI AWAMU YA SITA YAVUNJA REKODI BAJETI UNUNUZI WA DAWA,VIFAA TIBA | Tarimo Blog



Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Dodoma


Serikali imeweka rekodi katika ununuzi wa dawa kwa kutenga sh. Bilioni 200 katika bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 na kutoa sh. bilioni 140.9 sawa na asilimia 94 kati ya sh. bilioni 150 zilizotakiwa kutolewa hadi Machi.

Akizungumza leo mbele ya wahariri wa vyombo vya habari nchini katika semina kwa wahariri wa vyombo vya habari iliyoandaliwa na MSD, Mfamasia Mkuu wa Serikali Daud Msasi amesema hatua hiyo ni kubwa huku akifafanua kwamba serikali imeendelea kuimarisha upatikanaji wa fedha za kutosha kununua dawa.

Mbali na kupata bajeti kwa asilimia 94 na kufanya Serikali inayoongozwa na Rais Samia Dk. Suluhu Hassan na kuweka rekodi ya kutoa fedha nyingi kwa wakati, pia MSD imesambaza vifaa vya maabara, mashine za kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo na vyandarua vya wananchi.

"Mara moja moja huwa tunaona taarifa zikiripotiwa kuhusu haya, ni vyema sasa mkawapa fursa pia waandishi wanaowakilishwa na wahariri hawa kufika kuona namna wanachi wanavyofaidika na huduma hiyo," amesema.

Pamoja na hayo ametumia nafasi hiyo kuzungumzia umuhimu wa semina iliyoandaliwa na MSD kwa wahariri kwa ajili ya kukaa nao kuangalia namna ya kuboresha mawasiliano na niwapongeze pia wahariri kwa kukubali mwaliko mliopewa.

"Ninyi ni kundi muhimu kwa kutoa habari kwa jamii, kuelimisha umma, kulinda usalama wa nchi, kufichua uovu, kuchochea maendeleo na kulinda umoja wa kitaifa. Na katika kutekeleza haya, ni muhimu mkawa karibu na wadau wenu kufahamu wanafanya nini, wanakwama wapi, wanafanikiwa wapi, wanapinda wapi na wanakwenda wapi. Haya yote ndiyo jamii inataka kusikia, kuona mabadiliko na hatua za mafanikio.

"Wote tunafahamu kuwa kutokana na idadi ya wananchi kuongezeka nchini, Serikali imeongeza vituo vya kutolea huduma za afya kwakujenga vituo vipya na kupandisha hadhi vituo vya afya ili kuweza kupanua huduma za afya nchini.Maendeleo hayo yanapotokea MSD inakuwa na jukumu kubwa la kuhakikisha vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchi vinawezeshwa kupata bidhaa za afya ikiwa ni pamoja na vifaa tiba, mashine mbalimbali na dawa,"amesema.

Amesema ni vyema wahariri wafahamu kuwa MSD ndiyo Taasisi inayohusika na kununua, kuhifadhi na kusambaza bidhaa afya kwa kwa vituo vya umma vya kutolea huduma za afya nchini huku akifafanua mara kadhaa wamekuwa wakisikia malalamiko kadhaa yahusuyo bidhaa za afya.

"Aidha ni kukosekana ama kuchelwa, kwanini shida hii? Je, ni tatizo la MSD? ambayo inakiri kupokea fedha za kununulia bidhaa za afya kwa wakati ama kuna mambo mengine ambayo tunapaswa kuyafahamu? Basi katika siku mbili hizi lazima tufahamu vizuri masuala mazima ya mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya.

"Kama nakumbuka vizuri, Aprili, Mkurugenzi Mtendaji wa MSD anatimiza mwaka tangu ateuliwe kuingoza MSD, baadhi ya mafanikio tunayaona na kuyasikia kupitia vyombo vya habari vinavyoongozwa na hawa hawa wahariri.Nikupongeze ndugu Mavere kwa kutimiza mwaka, na umekuwa na ushirikiano na vyombo vya habari vya Dodoma, Dar es Saam na hata radio za kijamii huko mikoani,"amesema.

Pia amesema mafanikio au changamoto za sekta ya afya kwa namna moja ama nyingine yanahusiana na Bohari ya dawa (MSD) kwa asilimia kubwa." Leo tutahamu zaidi namna ya kupata taarifa zaidi za sekta ya afya kupitia MSD, kitaalam mnaita “angle” ama kupata viashiria mbalimbali vya habari.
Mfamasia Mkuu wa Serikali Bw. Daudi Msasi akieleza  kuhusu Serikali ilivyoweka rekodi katika ununuzi wa dawa kwa kutenga sh. Bilioni 200 katika bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 na kutoa sh. bilioni 140.9 sawa na asilimia 94 kati ya sh. bilioni 150 zilizotakiwa kutolewa hadi Machi,kwenye semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini iliyoratibiwa na Bohari ya Dawa(MSD) kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini.Picha na Michuzi Jr-MICHUZI MEDIA


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2