MKURUGENZI NEMC AKERWA NA KELELE CHAFUZI. | Tarimo Blog


Na Jane Edward, Arusha

Baraza la taifa na usimamizi wa mazingira NEMC limetoa miezi sita kwa wamiliki wa baa na kumbi za starehe pamoja na baadhi ya nyumba za starehe kote nchini yanayoendesha shughuli zao kwa kelele chafuzi majira ya usiku kuacha mara moja ndani ya kipindi hicho kwani serikali itaaza kuchukua hatua zidi yao.

Kauli hiyo imetolewa jijini Arusha na mkurugenzi mkuu wa NEMC nchini Dr.Samuel Gwamaka wakati alipotembelea moja ya kanisa lililopo mtaa wa Sama kata ya Moivo wilayani Arumeru linalotuhumiwa na wananchi kuendesha kelele chafunzi majira ya usiku bila kufuata sheria za mazingira.

Gwamaka amesema agizo hilo ni la miezi sita na ni kwa nchi zima kutekeleza sheria za mazingira na ndani ya kipindi hicho watakao kiuka tutawachukulia hatua ikiwemo kuwafungia hadi hapo watakapo kidhi vigezo vya mazingira.

"Sheria ziluzowekwa ni lazima ziheshimiwe kelele chafuzi zikiwepo zinasumbua wananchi wengine kwani kwenye jamii kuna watu mbalimbali ikiwemo wagonjwa"Alisema

Naye Mwenyekiti wa mtaa huo Baraka Shange pamoja na kupongeza juhudi za baraza la NEMC kufika katika mtaa huo amekiri kua hali ilikua mbaya ya kelele ambayo ilikua kero kwa wananchi wa maeneo hayo.

"sisi Kama wananchi wa mtaa huu tumekua tukilalamikia kelele ambazo zimekua zikizalishwa na kanisa hilo watu wanashindwa kulala nyakati za usiku lakini kwa sasa tunaimani kua ujio wa NEMC swala hili litamalizika"Alisema.

Mchungaji wa kanisa hilo Selestine Massawe pamoja na kupatiwa elimu ya mazingira na Baraza la Taifa na usimamizi wa mazingira Nemc ameahidi kufuata sheria pamoja na kutekeleza maagizo yote aliopatiwa na mkurugenzi mkuu wa Nemc.

"Nina ahidi kufuata maelekezo niliyopewa na NEMC ili kuweka mahusiano mazuri na jamii kwa kuwa natoa huduma za kimungu na migogoro haina afya "Alisema
Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dr Samuel Gwamaka akitoa somo la kelele chafuzi.

Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dr Samuel Gwamaka akizungumza na waandishi wa habari katika kanisa linalotajwa kufanya kelele chafuzi.
Mchungaji Selestine Massawe akitoa ufafanuzi juu ya uwepo wa kelele chafuzi kanisani hapo.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2