Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umetoa mafunzo kuhusu mradi wa Boresha Habari katika Chuo cha Uandishi wa Habari cha Rida ili kuhakikisha kuwa waandishi chipukizi wa vyuo vya vikuu na vyuo vya kati vinakuwa na uelewa hasa kwenye usawa wa kijinsia pamoja na uandaaji wa Bajeti yenye mlengo wa kijinsia.
Akizungumza wakati wa kutoa mafunzo Mratibu wa Mradi wa Boresha Habari Mariam Oushoudada amesema lengo la mradi huo ni kuhakikisha wanafunzi wa wanapata elimu ya kutosha kuhusu masuala ya uandishi wa habari wa Kijinsia pamoja na kujua jamii kwa ukaribu zaidi hasa wanawake, vijana na Watu wenye ulemavu kabla hawajaanza kuripoti habari.
Amesema lengo ni kuweza kuwainua wanawake kwenye masuala yote ya uongozi pamoja na kujitambua kwani wanawake wengi bado hawana ujasili wa kuwawania nafasi kwani bado hawajapewa elimu ya kutosha hivyo mradi huu umekuja kwenye wakati mzuri hasa kwa wanachuo wa wanaosomea tasnia hiyo kwani watakuwa mabalozi wazuri.
Pia amasema mradi huu ni wa miezi minne ambapo lengo kuu ni kuvifikia vyuo 10 vya kati na vya juu vinavyotoa taaluma ya Habari vilivyopo kwenye mikoa ya Pwani na Dar es Salaam ambapo itaandaa tuzo kwa waandishi ili wawezesha wanafunzi hao wanapomaliza Masomo kuweza kuandika habari sahihi na zilizokuwa na usawa ambazo zinakuza ushiriki, ujumuishaji, na uwajibikaji kwenye mlengo wa Kijinsia.
Mratibu wa Mradi wa Boresha Habari Mariam Oushoudada akitoa maelezo kuhusu mradi huo kwa wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari cha Rida waliofika kwenye mafunzo yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) kwa kushiriikiana na chuo hicho kilichopo Tabata Segerea Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Mwezeshaji kutoka TGNP Catherine Mzurikwao akitoa maelezo kuhusu namna mtoto wa kike anavyoweza kijisimamia pamoja na kazi zinazofanywa na huo Jinsia Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa baadhi ya Chuo cha Uandishi wa Habari cha Rida kilichopo Tabata Segerea Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanachuo wa Chuo cha Uandishi wa Habari cha Rida waliofika kwenye mafunzo wakifuatilia mada zilizokuwa zinatole na watoa mada kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) hasa kwenye masuala ya kijinsia wakati wa mafunzo ya mradi wa Boresha Habari yaliyofanyika katika chuo hicho kilichopo Tabata Segerea Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment