Jumla ya Wakufunzi 13 kutoka Taasisi mbalimbali za Usafiri wa Anga nchini wamefaulu kozi namba 23 ya kuwajengea uwezo walimu katika Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC).
Akizungumza wakati wa kufunga kozi hiyo Mkufunzi Mkuu wa kitengo cha Uongozaji Ndege, Godlove Longole aliyemwakilisha Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC) Aristid Kanje amesema lengo la kozi hiyo ni kuwawajengea uwezo wakufunzi ili wanapotoa mafunzo yawe yenye tija kwa wanafunzi.
Pia Longole amewapongeza washiriki wa kozi hiyo kwa juhudi zao zilizowawezesha darasa zima kupata vyeti vya kumaliza badala ya vyeti cha kushiriki kozi hiyo vizuri ikiwa na ufaulu mzuri.
Wakufunzi hao wa kozi hiyo iliyoanza Januari 15 hadi Januari 26, 2024 ni kutoka Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa Anga (TCAA -CCC).
Mkufunzi Mkuu wa kitengo cha Uongozaji Ndege, Godlove Longole akizungumza wakati wa kufunga kozi ya Wakufunzi iliyokuwa na lengo la Kuwajengea Uwezo walimu hao kwenye mahafali iliyofayika katika chuo cha cha Usafiri wa Anga nchini(CATC).
Mkufunzi mkuu wa Kitengo cha Kuendeleza Mitahala (CATC) Neema Senyagwa akitoa utambulisho pamoja na kueleza dhumuni ya mahafali hayo kwa Mkufunzi Mkuu wa kitengo cha Uongozaji Ndege, Godlove Longole aliyemwakilisha Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga nchini(CATC) Aristid Kanje katika mahafali ya kozi ya Wakufunzi yaliyofanyika katika chuo hicho jijini Dar es Salaam
Mwalimu kutoka Chuo cha Usafiri wa Anga nchini(CATC) Dkt. Daniel Kerenge akitoa maelezo kuhusu namna alivyotoa elimu kwa wakufunzi waliohudhulia kozi ya 23 katika chuo hicho wakati wa mahafali ya kozi ya Wakufunzi yaliyofanyika katika chuo hicho jijini Dar es Salaam
Baadhi wa Wahitimu wa Kozi ya 23 wakifatilia hotuba ya Mkufunzi Mkuu wa kitengo cha Uongozaji Ndege, Godlove Longole aliyemwakilisha Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga nchini(CATC) Aristid Kanje katika mahafali ya kozi ya Wakufunzi yaliyofanyika katika chuo hicho jijini Dar es Salaam
Picha ya pamoja
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment