SHIRIKA LA NDEGE LA EMIRATES KUBADILISHA RATIBA YA SAFARI SASA NI BURE..... | Tarimo Blog

SHIRIKA la ndege la Emirates limeanzisha sera mpya za nyongeza  zitakazowapa uhuru wateja wao katika kupata huduma za usafiri.

Shirika hilo limekuja na sera hizo kwa kuwakarimu wateja kwa kutoa machaguo zaidi katika kupanga mipango ya safari zao.

Imeelezwa kuwa shirika hilo limewapa uwezo wateja kubadili tarehe za safari zao bila makato kuanzia Machi 7 hadi 31 mwaka huu.

Pia imeelezwa kuwa wateja wa Emirates wanaweza kubadilisha ratiba za safari zao na hiyo ni kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona (Covid 19) na wateja watakuwa huru kubadili tarehe za kusafiri ndani ya miezi 11 kwa daraja lilelile bila makato yoyote na sera hiyo mpya inahusisha maeneo yote ambayo yana mtandao wa Shirika hilo la Emirates.

Afisa Mkuu wa biashara wa Emirates Adnan Kazim amesema kuwa,
"Tunapenda wateja watu wajisikie wakiungwa mkono kikamilifu wakati wa kupanga mipango yao ya kusafiri kwa kulipa nauli zao na kufanya mabadiliko bila ada ya ziada" Ameeleza.

Amesema kuwa ikiwa wateja watabadili tarehe za kusafiri wataendelea kutafuta njia faafu, rahisi na zitakazowaridhisha wateja.

Pia imeelezwa kuwa shirika hilo lipo makini katika katika kuchukua tahadhari kufuatia mlipuko wa virusi vya Covid 19 na hiyo ni pamoja na kuweka mchakato wakusafisha ndege zote kwa kemikali Kali zilizoidhinishwa, na kuelezwa kuwa ikiwa itaarifiwa kuwa na kesi yoyote iliyothibitishwa hatua madhubuti zitachukuliwa.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2