HALMASHAURI WILAYA YA MERU MKOANI ARUSHA YATUMIA MILIONI 308/_ KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO HADI KUFIKIA APRILI 15 | Tarimo Blog

Na Woinde Shizza ,MERU

HALMASHAURI ya Wilaya ya Meru mkoani Arusha imetumia zaidi ya shilingi milioni 308 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika kipindi Cha mwaka wa fedha 2019//2020 hadi kufikia Aprili 15 mwaka huu.

Akizungumza leo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru Emmanuel Mkongo amesema kuwa halmashauri hiyo katika kuunga mkono jitihada za wananchi kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020 ilitenga kutoka katika makusanyo ya mapato ya ndani jumla ya shilingi milioni 515.


Na kutumia shilingi milioni 308 katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ununuzi wa vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vyumba 21 vya madarasa na vyumba 3 vya maabara sambamba na ununuzi wa viti na meza

Amesema kuwa ikiwa ni mkakati wa Halmashauri hiyo kuendelea kuboresha miundombinu ya sekta ya elimu kwa kukamilisha vyumba vya madarasa na maabara ili kutatua changamoto ya msongamano wa wanafunzi kutokana na ufaulu mkubwa wa wanafunzi walioingia kidato cha kwanza mwaka huu na mkakati wa kuboresha ufundishaji wa masomo ya Sayansi.

Aidha , akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya Sh. 18,961,020.06 kwa Shule ya Sekondari Maroroni na Sing'isi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na maabara, Mkongo amesema vifaa hivyo vimegawanywa kwenye Kata zote 26 kwa kutoa kipaumbele kwa Kata ambazo Wananchi wake wameonesha juhudi za kuchangia ujenzi wa miradi ya maendeleo akitolea mfano Kata ya Maroroni na Sing'isi na kutoa wito kwa wananchi wa Kata nyingine kufanya vizuri zaidi.


Ameongeza kuwa fedha hizo jumla ya Shilingi milioni 308 za mapato ya ndani ya Halmashauri na Shilingi 50,666,300 za mfuko wa kuchochea maendeleo ya jimbo ambao Mwenyekiti wa Kamati ya ya Mfuko huo ni Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Dkt. Danielson Pallangyo zimechochea kwa kiasi kikubwa ujenzi na ukamilishaji wa Miundombinu hiyo.

Aidha, Mtendaji wa Kata ya Maroroni Lyidia Sarakikya amemshukuru Mbunge Dkt.Pallangyo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa kutoa mbao, bati na mifuko ya saruji kwaajili ya kukamilisha vyumba 3 vya madarasa kwani imewatia wananchi moyo kwa kupunguza ukali wa michango.

Wakati huo Mkuu wa Shule ya sekondari Maroroni Mwalimu Felix Nibigira aliishukuru Serikali na kutumia fursa hiyo kutoa wito kwa wazazi kutokubweteka kipindi ambacho shule zimefungwa badala yake wawasimamie wanafunzi kufanya mazoezi yaliyotolewa kwani shule hiyo iliwaandalia majaribio na masomo kwa kifurushi kilichopewa jina la HOME PACKAGE.
 Picha Mwonekano wa Vyumba 2 vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Maroroni iliyopokea vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 11  ikiwa ni mifuko ya saruji 50,mbao  zenye thamani ya milioni 6,201,000  na bati  110.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2