NAIBU WAZIRI ABDALLAH ULEGA ATOA POLE KWA FAMILIA 21 AMBAZO NDUGU ZAO WAMEFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BASI MKURANGA | Tarimo Blog

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega ametoa pole kwa familia 21 zilizopata msiba uliotokana na ajali ya basi iliyotokea maeneo ya kilimahewa wilayani Mkuranga mkoani Pwani na kuwataka wananchi kuchukua taadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona.    
                                           
Akizungumza na wanafamilia hao aliowatembelea kuwapa pole katika kata saba za Wilaya ya Mkuranga, Ulega aliwapatia kiasi zaidi ya Sh.milioni moja na unga kwa familia hizo za marahemu.       
                                
Aidha Ulega amesema amesikitishwa na msiba huo na kuwataka wafiwa wote kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu.   "Nchi yetu hipo katika janga la corona kwahiyo tuchukue tadhari Kwa kufuata maelekezo yanayotolewa na serikali."      

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkuranga Juma Athuman Abeid amesema watafatilia ili kuhakukisha watu wote waliopata ajali wanapata haki zao kupitia bima.
Naibu Waziri wa Mifugo na  Uvuvi  mbunge  wa Mkuranga mkoa Pwani Abdallah Ulega  (wapili kulia) akiwa ameambatana na ziongozi mblimbli wa wilaya hiyo wakielekea kata ya Magawa  kuwapa pole  wanafamilia waliopatwa na  msiba uliotokana na ajali ya basi iliyotokea maeneo ya kilimahewa wilayani Mkuranga mkoani Pwani.Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv) 
 Naibu Waziri wa Mifugo na  Uvuvi  mbunge  wa Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega (kulia)akiwapa pole wanafamilia waliopatwa na  msiba uliotokana na ajali ya basi iliyotokea maeneo ya kilimahewa wilayani Mkuranga mkoani Pwani,(katikati) ni Mwenyekiti wa halmashaul ya Wilaya Mkuranga na Diwani wa kata ya Magawa,Juma Abed
 Naibu Waziri wa Mifugo na  Uvuvi  mbunge  wa Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega (kushoto)akiwapa pole  wanafamilia waliopatwa na  msiba uliotokana na ajali ya basi iliyotokea maeneo ya kilimahewa wilayani Mkuranga mkoani Pwani,ambapo aliwaomba wananchi kuchukua taadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona.    
 Mwenyekiti wa halmashaul ya Wilaya Mkuranga na Diwani wa kata ya Magawa,Juma Abed (alievaa  kanzu) akiwapa pole  wanafamilia waliopatwa na  msiba uliotokana na ajali ya basi iliyotokea maeneo ya kilimahewa wilayani Mkuranga mkoani Pwani,ambapo amesema watafatilia ili kuhakukisha watu wote waliopata ajali wanapata haki zao kupitia bima.

Naibu Waziri wa Mifugo na  Uvuvi  mbunge  wa Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega (kulia) akiongoza dua ya kuwaombea marehemu katika ajali ya basi iliyotokea maeneo ya kilimahewa wilayani Mkuranga mkoani.










Naibu Waziri wa Mifugo na  Uvuvi  mbunge  wa Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega ametoa pole kwa familia 21 zilizopata msiba uliotokana na ajali ya basi iliyotokea maeneo ya kilimahewa wilayani Mkuranga mkoani Pwani.(Picha zote na Emmanuel Massaka,Michuzi Tv)



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2