Na Amiri kilagalila,Njombe
Watanzania wametakiwa kuona fursa zilizopo nchini na kutumia ubunifu walionao ili kuzitumia rasilimali hususani madini yaliyopo nchini na kuinuka kiuchumi.
Wito huo umetolewa na Prof.Silvester Mpanduji mkurugenzi mkuu wa shirika la viwanda vidogo (SIDO) na mwenyekiti wa kamati ya wajumbe tisa kutoka wizara nne,wizara ya madini,wizara ya nchi ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira,wizara ya viwanda na biashara pamoja na wizara ya ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (OR-TAMISEMI) iliyoundwa na waziri wa madini Doto Biteko na kufika mkoani Njombe ili kuangalia shughuli anazozifanya Reuben Mtitu (mzee Kisangani) katika uyeyushaji wa chuma na jinsi ya kumsaidia.
“Tumekuja kuangalia shughuli anazozifanya mzee Kisangani lakini kikubwa ni kuangalia ni jinsi gani tunaweza tukamkuza kutoka hapa alipo na kuhakikisha anakuwa na kiwanda na kikubwa”alisema Prof.Silvester Mpanduji
Pia amesema ipo fursa kubwa kwa vijana kuiga kutokana na shughuli za uyeyushaji chuma unaofanywa na mzee Kisangani kwa ajili ya kuzalisha bidhaa mbali mbali kama vile nyundo,majembe,fyekeo na visu
“Kweli tumeshuhudia mkoa wa Njombe una rasilimali nyingi za madini na wengi wakiweza kuiga nadhani tutakuwa na viwanda vidogo vidogo ambavyo vinachakata haya madini na kupelekwa kwenye viwanda vyetu badala ya kuagiza chuma kutoka nje,kwa hiyo kwa vijana ni fursa kubwa kuiga anavyofanya mzee Kisangani”alisema tena Prof.Silvester Mpanduji
Akizungumza mbele ya kamati hiyo iliyotembelea ofisi zake za utengenezaji mageti,visu,shoka,mapanga na hata majembe iliyopo Njombe mjini, Reuben Mtitu maarufu mzee Kisangani huku akionekana kuwa mwenye bashasha amesema ni furaha kubwa kwake kuona serikali inawajibika kuwasaidia wajasiriamali wadogo wenye ubunifu na mtizamo chanya kuikuza sekta ya viwanda nchini huku akitoa baadhi ya bidhaa kama zawadi kwa waziri biteko.
“Ninamshukuru sana waziri Biteko kwa kutembelea mradi wangu kule shambani na baadaye kutuma timu ya wataalamu na kuja kunitembelea mpaka kuona workshop,mimi kweli naahidi kuingia kwenye utekelezaji zaidi na aahidi kujituma kwenye kazi maana serikali imeamua kunisaidia,na nitawashawishi vijana wangu niliyowafundisha kuingia kwenye chuma kwasababu kuna ajira kubwa zaii”alisema Mzee Kisangani
Issah Mtuwa ni afisa mawasiliano wizara ya madini amepokea zawadi ya Sululu,kisu na nyengo zinazotengenezwa na mzee huyo kwaniaba ya Waziri Biteko na anasema kama wizara itaendelea kuwainua wabunifu wote walioko nchini lengo likiwa ni kuwapa fursa wabunifu wadogo waweze kutekeleza na kufikia malengo yao, mathalani tuifikie Tanzania ya viwanda.
“Nadhani mtakumbuka waziri Biteko amekuja mara kadhaa kwa ajiri yam zee Kisangani,na dhamira yake juu ya ubunifu wa mzee huyu hata alipokuja tarehe 13 mpaka 16 aliongea mengi ambayo mzee huyu ameyasema na mzee amekili kusaidiwa kwa muda mfupi,nimepokea zawadi alizotoa na mimi nitafikisha na kama tunavyoona kamati imetembelea eneo la kiwanda na eneo la uzalishaji lengo la serikali likiwa ni kuinua watu wenye ubunifu kama alivyo sema Rais Magufuli kuwa yupo tayari kuwasaidia kila anayeonyesha ubunifu hasa kwenye viwanda”alisema Issa Mtuwa
Katibu wa wachimbaji wadogo wa madini mkoa wa Njombe Isaya Mhagama kwaniaba ya wachimbai wa madini amempongeza waziri Biteko kwa hatua kubwa alizozichukua ili kumsaidia mbunifu huyu maarufu kwa jina la Kisangani.
“Tunamshukuru sana waziri Biteko lakini pia katika ombi letu kwa kuwa mkoa wa Njombe unaweza kutengeneza madini ya viwanda tutahakikisha na pia tunaweza kushindana na mikoa mingine yenye madini kwa hiyo tunaiomba serikali na wizara izidi kutuangalia”alisema Isaya Mhagama
Mbunifu Reuben Mtitu ameajiri na kuwafundisha vijana zaidi ya 120 ambao wamepewa mafunzo ya uyeyushaji chuma na utengenezaji wa bidhaa kama mapanga , Visu , Shokana na Nyundo bila malipo ya yoyote na kuendelea na shughuli zao pia katika maeneo mengi mkoani Njombe. Lakini hata hivyo serikali kupitia wizara ya madini imeanza kutatua baadhi ya changamoto kama ukosefu wa makaa ya mawe kwa ajili ya uyeyushaji chuma katika shughuli za mzee huyo ambapo kampuni ya uchimbaji wa madini ya makaa ya mawe TANCO imeweza kumkabidhi tani 30 za makaa yam awe ili kuondokana na changamoto hiyo.
Reuben Mtitu maarufu mzee Kisangani huku akionekana kuwa mwenye bashasha wakati kamati hiyo ilipofika kumtembelea katika eneo lake la kazi.
Kushoto ni Issah Mtuwa afisa mawasiliano wizara ya madini akipokea zadi ya mbali mbali ikiwemo nyengo kutoka kwa mzee Kisangani kwa ajili ya waziri Biteko
Katibu wa wachimbaji wadogo wa madini mkoa wa Njombe Isaya Mhagama akimshukuru waziri Biteko kwa niaba ya wachimbaji wadogo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment