Ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za kupambana na homa ya mapafu maarufu kama Corona virus, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imeshirikiana na Wizaya ya Afya Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kusambaza vipeperushi vyenye ujumbe wa kujikinga na virusi hivyo hatari
SBL tayari imeshavifikisha vipeperushi hivyo sehemu mbali mbali hapa nchini na kuvikabidhi kwa Waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na maafisa afya kwa ajili ya kuvigawa kwa wanachi wa maeneo husika.
Mwakilishi wa mauzo wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) mkoa wa Lindi Anna Msomba (kushoto) akikabidhi sehemu ya vipeperushi vyenye ujumbe wa namna ya kujikinga na virusi hatari vya Corona kwa Afisa Afya wa mkoa huo Richard Shaban. Kampuni ya SBL imejitolea kwa kushirikiana na Wizaya ya Afya kusambaza vipeperushi hivyo sehemu mbali mbali nchini. Kulia ni Damasiana Msala kutoka kitengo cha uuguzi cha hospital ya mkoa huo, Sokoine.
Mwakilishi wa mauzo wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) mkoa wa Tanga George Rweyemamu (kulia) akikabidhi sehemu ya vipeperushi vyenye ujumbe wa namna ya kujikinga na virusi hatari vya Corona kwa Mohamed Khalifa ambaye ni mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa huo. Kampuni ya SBL imejitolea kwa kushirikiana na Wizaya ya Afya kusambaza vipeperushi hivyo sehemu mbali mbali nchini.
Mwakilishi wa mauzo wa Kampuni ya Bia ya Seerengeti (SBL) mkoa wa Kagera Laurent Nditi (kulia) akikabidhi sehemu ya vipeperushi vyenye ujumbe wa namna ya kujikinga na virusi hatari vya Corona kwa Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dkt Hassan Kawia. Kampuni ya SBL imejitolea kwa kushirikiana na Wizaya ya Afya kusambaza vipeperushi hivyo sehemu mbali mbali nchini.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment